VATICAN CITY, VATICAN
RAIS wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amekutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, ikiwa ni ziara ya kwanza kwa kiongozi wa Uturuki kuzuru Vatican kipindi cha karibu miaka 60 iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais Erdogan, viongozi hao walijadili mgogoro kuhusu Jerusalem, uhusiano kati ya Uturuki na Vatican, mgogoro wa wakimbizi na ugaidi.
Papa Francis ni miongoni mwa viongozi ambao wamekuwa wakipaza sauti kukosoa hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.