25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

SHINIKIZO LAZIDI KUMKABILI ZUMA AJIUZULU

PRETORIA, AFRIKA KUSINI


CHAMA tawala cha African National Congress (ANC), jana kiliitisha kikao cha dharura kujadili hali ya baadaye ya Rais Jacob Zuma, baada ya mazungumzo ya juzi usiku kushindwa kumshawishi ajiuzulu.

Zuma, ambaye  yuko  madarakani  tangu mwaka 2009, kutokana na kashfa za ufisadi amekuwa akizidi kubanwa kumtaka ajiuzulu tangu nafasi yake ya kuiongoza ANC ilipochukuliwa na makamu wake, Cyril Ramaphosa Desemba mwaka jana.

ANC iliitisha  kikao cha Kamati  ya Taifa  ya  Utendaji  kukutana  katika  makao  makuu  ya  chama hicho, Luthuli House jijini  Johannesburg kwa  majadiliano.

Ili  chama  hicho  kiweze  kumlazimisha  Zuma  kujiuzulu nafasi yake ya rais wa nchi, kamati  hiyo italazimika  kuitisha  mkutano  wa  Kamati Kuu  ya  Taifa, ikiwa  ni  chombo  chake  kikuu  cha  uamuzi, kupiga kura kumwondoa  Zuma.

Maofisa  sita  wa  ngazi  ya  juu  wa  ANC,  walikutana na  Zuma  usiku  wa juzi katika  makazi yake mjini Pretoria, lakini hakuna  taarifa iliyotolewa kuhusu kikao hicho.

Kiongozi  wa  upinzani,  Julius Malema, mwanachama  wa  zamani wa ANC, alisema  Zuma amegoma kujiuzulu.

“Amekataa  kujiuzulu  na  aliwaambia  wachukue  uamuzi  kumwondoa iwapo wanataka  kufanya  hivyo,  kwa sababu  hajafanya  lolote baya  kwa  nchi,” Malema aliandika  katika  ukurasa  wa Twitter.

Zuma ametengwa na  washirika  wake  muhimu tangu  Ramaphosa achaguliwe kuongoza chama  pekee kuiongoza Afrika Kusini tangu  kumalizika kwa utawala wa Wazungu  wachache  mwaka 1994.

Ramaphosa (65) yuko katika nafasi nzuri  ya  kuwa rais ajaye na amekuwa akiingiza ushawishi wake ili Zuma aondolewe madarakani.

Zuma hajasema iwapo atajiuzulu kwa hiari kabla ya muda wake wa muhula wa pili kumalizika mwakani.

Vyama vya upinzani na baadhi ya wanachama wa ANC, wanataka aondoke kabla ya hotuba  ya hali ya taifa hilo katika Bunge, iliyopangwa  kutolewa  hapo Alhamisi.

Zuma anastahili kusalia madarakani hadi uchaguzi wa mwakani, lakini chini yake chama kimepoteza umaarufu, uchumi ukidorora na tuhuma za rushwa zikikithiri.

Kwa sababu hiyo, viongozi wanataka aondoke mapema kabla ya uchaguzi huo, kusafisha taswira ya chama mapema na kukijengea upya sifa yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles