30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

PUTIN ACHEKELEA NDEGE YENYE NGUVU KIVITA

MOSCOW, URUSI


RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amesema ndege mpya ya kimkakati ya kivitta, New Tupolev Tu-160 itaimarisha sekta ya nyuklia ya taifa lake.

Putin alisema hayo wakati akiangalia ufanisi kiutendaji na umahiri wa ndege hiyo kubwa, ambayo ni moja ya zenye nguvu zaidi duniani jijini Kazan juzi.

“Hii ni hatua muhimu ya maendeleo ya teknolojia yetu na kuimarisha uwezo wa kujilinda wa taifa,” alisema Putin wakati akizungumza na wafanyakazi wa Kiwanda cha kutengeneza ndege cha Gorbunov jijini humo.

Rais Putin aliisifu menejimenti ya kiwanda hicho kwa mafanikio makubwa ya utengenezaji ndege zenye teknolojia ya hali ya juu katika medani ya kivita.

Akizungumzia kuhusu ofa ya kutembelea ndege hiyo kwa mwaka mmoja na nusu, Putin alisema haina haja kwa sababu alishafanya hivyo katika toleo lililotangulia la ndege hiyo.

Kwa mujibu wa Putin, hana shaka na utaalamu uliotumika kuutengeneza mradi huo wa Tu-160, akisema anaamini utaenda vyema.

Lakini pia kwa mara nyingine alisisitiza umuhimu wa kuimarisha usafiri wa anga, hasa kwa kutengeneza toleo la ndege ya kiraia la Tu-160.

“Nafahamu ndege hiyo inahitaji juhudi nyingi kuitengeneza, lakini itakuwa na mahitaji makubwa duniani,” aliongeza Putin.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles