25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MARAFIKI WAJIGUNDUA NI NDUGU WA DAMU BAADA YA MIAKA 60

INAKUWAJE unapokuja kubaini kuwa rafiki yako wa ‘kufa na kuzikana’ wa miaka mingi kumbe ni nduguyo wa damu?

Bila shaka unapata msisimko wa aina yake, kubwa ukiwa wa furaha unayoweza kuifananisha na moja ya zawadi nzuri zaidi kuwahi kuzipata maishani mwako.

Ndivyo ilivyowatokea wakazi hawa wawili wa Hawaii nchini Marekani, lan Robinson na Walter MacFarlane, baada ya kugundua hilo siku chache kabla ya Sikukuu ya Krismasi mwaka jana.

Waligundua kuwa wanahusiana baada ya kila mmoja kwa wakati wake kwenda kuchukua vipimo vya vinasaba (DNA).

Lengo lao lilikuwa si kupata ukweli kuhusu uhusiano wao kwa vile hawakuwa na wazo hilo bali kupata maelezo yatakayomsaidia kila mmoja kumpa mwanga wa wapi anakotokea.

Ni kwa vile wote waliasiliwa wakati wakiwa wadogo na hivyo kutowafahamu vilivyo wazazi wao.

Marafiki hao wa zaidi ya miongo sita walishtushwa wakati walipobaini bila kutarajiwa kuwa ni mtu na kaka yake, miaka 60 sasa tangu wafahamiane.

Alan Robinson na Walter MacFarlane wamefahamiana tangu walipoanza shule moja ya msingi huko Hawaii.

Ni kutokana na ukubwa wa urafiki wao, waliwapeleka watoto wao kuanza shule katika shule hiyo hiyo ya msingi waliyosoma wao hapo Hawaii miaka 60 iliyopita.

Na kudhihilika kushibana wamekuwa wakienda likizo kutembelea miji au nchi mbalimbali wakiungana pamoja na wake na watoto wao.

MacFarlane (74) kamwe hakuwahi kuonana na baba yake wakati Robinson (72) aliasiliwa na hawafahamu kabisa wazazi wake kamili. Lakini kwa sasa wameshtushwa kufahamu kuwa wamechangia mama mmoja.

Wote wakifanana kuwa na tatizo la kutowajua wazazi wao, wakiwa hawana wazo kuwa wanafahamiana, kila mtu kwa wakati wake akaamua kusaka kizazi chake.

MacFarlane baada ya majibu ya vipimo alitumia tovuti ya kulinganisha DNA yake na kubaini inafanana na ya mtu mwenye ‘X chromosomes’ anayetumia jina Robi737.

Robinson, rubani wa zamani wa Shirika la Ndege la Aloha nchini humo, alitumia tovuti hiyo hiyo.

Kaka hao wa mama mmoja, baba tofauti kwa sasa wameanika ugunduzi wao huo kwa marafiki na familia zao.

Robinson anasema: “Hii ni zawadi nzuri kabisa ya Krismasi, ambayo sikuwahi kuwaza kuipata.

“Nilikuwa na mdogo wangu niliyempoteza wakati akiwa na miaka 19, hivyo sikuwa na binamu wala nini.

“Nilidhani kwamba sitoweza kumjua mama yangu mzazi.

Macfarlane alizaliwa mwaka 1943 huko Honolulu. Mama yake Genevieve, alikuwa akipanga kumwasili, lakini wazazi wake waligundua hilo, wakaamua kumuasili kwa utaratibu usio rasmi mjukuu wao huyo.

Miezi 15 baadaye Robinson akazaliwa katika mji huo huo na mara moja alikabidhiwa kwa familia nyingine na kamwe hakuwajua wazazi wake waliomzaa.

Wanaume hao walikutana tu wakati walipojiunga shule ya msingi wakiwa watoto na kuanzia hapo wakawa marafiki wakubwa hadi leo hii, ambao familia zao zi karibu mithiri ya ndugu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles