23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MERKEL: KUJITENGA SI JIBU LA MATATIZO

DAVOS, USWISI


KANSELA wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema suala la kujitenga si jawabu la kutatua matatizo na changamoto za kiuchumi zinazoikabili dunia.

Akizungumza katika Kongamano la Kiuchumi la Kimataifa (WEF) mjini hapa, Kansela Merkel alisema yuko wazi kuhusu aina ya ushirikiano, ambao Umoja wa Ulaya (EU) itauendeleza baada ya Uingereza kujiondoa kutoka umoja huo.

Hata hivyo, alisema huenda pasiwepo maelewano kuhusu kanuni za msingi za EU katika mazungumzo na Uingereza, licha ya kuwa wanataka ushirikiano wa karibu na taifa hilo.

“Ujerumani inapenda kuwa nchi ambayo itatoa mchango wake, pia katika siku zijazo katika kutatua kwa pamoja matatizo ya dunia. Tunadhani kujitenga na wengine duniani hakutatuongoza na kutupeleka katika mustakabali mzuri. Kujitenga si jibu sahihi,” alisema Merkel.

Merkel pia alisema siasa za kizalendo zinazofanywa na wanasiasa wanaofuata siasa kali za mrengo wa kulia barani Ulaya, ni sumu inayochangia katika matatizo ambayo hayatatuliki, hivyo inapaswa kudhibitiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles