Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kamati hiyo pia imeelezwa kuwa mwekezaji katika mradi wa uwekezaji wa Mlimani City alikuja na mtaji wa Dola za Marekani  75 (Sh 150,000) kuwekeza katika mradi huo.
Kamati hiyo ambayo iko katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali pia imebaini madudu katika mradi huo na kuagiza wote waliosaini mkataba huo waitwe na kuhojiwa.
Aidha, kamati hiyo imeshangazwa na hatua hiyio na kuhoji taaaisi kubwa kama ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM) inayoaminika ndani na nje ya nchi ilishindwaje kukopa fedha za kuendesha mradi huo hadi kukubali mwekezaji wa aina hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Naghenjwa Kaboyoka, amesema kuna vitu vingi vimejificha katika mkataba huo hivyo ni lazima kuwe na watu  watakaowajibika.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye amekiri mkataba huo kuwa na matatizo hivyo wanachukua hatua kuyatatua.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Utawala, Profesa David Mfinanga, amesema wameunda kamati kupitia upya mkataba huo.