Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
RAIS Dk. John Magufuli, ameagiza kuchukuliwa hatua dhidi ya viongozi na watendaji ambao shule za msingi na sekondari zilizopo katika maeneo yao zinawatoza wanafunzi michango mbalimbali kinyume na mwongozo wa Serikali wa utoaji elimu bila malipo.
Agizo hilo amelitoa Ikulu Dar es Salaam jana, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo.
Alisema Serikali inatoa Sh bilioni 23.875 kila mwezi kuwezesha utoaji elimu bila malipo, lakini alishangazwa kuona bado kuna walimu wanaendelea kuwatoza michango ama kuwarudisha nyumbani wanafunzi ambao wanashindwa kutoa.
“Nawaagiza mawaziri, sitaki kusikia mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa kushindwa kutoa michango, na fikisheni maagizo haya kwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi, na wote wanaohusika. Nikisikia tena mahali jambo hili linaendelea, hawa niliowateua mimi wataondoka.
“Haiwezekani tumefuta ada, halafu walimu wanaamua kuanzisha michango, tena mikubwa ambayo watu masikini wanashindwa kusomesha watoto wao, na kama wazazi wanataka kuchangia kitu shuleni, wapeleke michango yao kwa mkurugenzi, lakini sitaki kusikia mwanafunzi anapewa sharti la kutoa mchango ndipo apokelewe shule,” alisema.
Rais Magufuli alitoa maagizo hayo baada ya kupata taarifa kuwa zipo baadhi ya ……………………….
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.