Hatua ya aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia kujivua uanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) jana, inadaiwa ni ahadi aliyopewa ni kulipiwa madeni yanayomuandama.
Hali hiyo inadaiwa kufikia hatua ya kutishiwa kunyang’anywa baadhi ya mali zake kutokana na kushindwa kulipa madeni hayo yanayodaiwa kuwa mengi.
Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumapili Desemba 3, kuhusu tuhuma hizo Mtulia amesema hayo ni ‘mapovu’ yanawasumbua kwani ameamua mwenyewe.
Alipoulizwa ni kwa nini kila kiongozi au mwanachama akitoka upinzani anasema ni kwa sababu anaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli kwa utendaji wake alisema ni kweli lazima iwe hivyo kwa kuwa Magufuli ndiyo kiongozi wa chama na mtekelezaji wa kila shughuli ndani ya chama.
“Hivi unafikiri inakuwa kwa ajili ya nani ni Magufuli kutokana na utendaji wake na ndio msimamizi mtekelezaji Wa shughuli zote ndani ya chama changu nilichokiona kinafaa ,hakuna mwingine ni yeye na huwezi kukwepa kumpa sifa hizo,” amesema Mtulia.
Kuhusu kugombea jimbo hilo kwa tiketi ya CCM alikohamia amesema: “itategemea na shughuli nitakayopangiwa na wakubwa wangu,”.
Akizungumzia suala hilo, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Joram Bashange amesema wamelipokea kwa shangwe na wanawaombea Mungu waende mapema wasiendelee kukivuruga chama.
“Hawa wamepandikizwa kwenye chama chetu pamoja na Lipumba walikuwa wakisaidiwa na Dola katika kuharibu chama. Huo ni mkakati wao kwa hata hakuandika barua kapitia katika mtandao wa kijamii, na bado kuna wenzake nao watakwenda huko, tulishajindaa na tunashukuru Mungu waende mapema.