24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

NASSARI AMZIKA MBWA WAKE KWA HESHIMA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), ameamua kumzika kwa heshima mbwa wake aliyeuawa kwa kupigwa risasi kwa kuokoa maisha yake.

Mbwa huyo alifariki usiku wa kuamkia jana, nyumbani kwa mbunge huyo katika Kijiji cha Nkwanenkori wilayani Arumeru, baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana ambao walimuua mbwa huyo kwa risasi.

Akizungumza na Mtanzania Digital, mbunge huyo amesema kwa kushirikiana na wananchi wa jimbo lake na viongozi mbalimbali wa Chama hicho, wamemzika mbwa huyo jana saa 10 jioni katika shamba lililopo karibu na nyumbani kwake.

“Nimeamua kumzika mbwa huyo kwa heshima kwani risasi zilizomuua pengine zingeingia mwilini mwangu na kuniua. Nimeimarika niko sawa namshukuru Mungu niko hai napumua hilo ndiyo kubwa kuliko yote.

“Tulishauriana tumzike vizuri kwa heshima zote kwa sababu kiukweli alipambana ndiyo maana akauawa na kama asingeuawa yeye ningeweza kuuawa mimi, naamini amechukua risasi ambazo pengine zingeingia kwenye mwili wangu, ni kama mwanajeshi ambaye amefia vitani akimpigania bosi wake, kwani baada ya kusikia milio ya risasi nje ilinichukua muda mrefu kutafuta silaha yangu hadi kutoka nje,” amesema Nassari.

Amesema wamemzika kwa majonzi kwani amekufa akilinda maisha yake na hakustahili kifo hicho ila naamini Mungu anaweza kumsaidia mtu kwa kutumia kitu chochote ambapo pia amemshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ambaye mbali na kumpa pole amemshauri kujiongezea ulinzi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles