29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

SANTOS AZISIKITIKIA MOROCCO, IRAN KOMBE LA DUNIA

LISBON, Ureno

KOCHA wa timu ya Taifa ya Ureno, Fernando Santo, amesema ni kikosi chake na Hispania ndicho kitakachofuzu hatua ya 16 bora ya fainali za mwakani za Kombe la Dunia na akaongeza kwamba, anazionea huruma Morocco na Iran.

Kauli yake inakuja baada ya droo ya hatua ya makundi kuchezeshwa juzi jijini Moscow, Urusi, ambapo mataifa hayo manne yalipangwa Kundi B.

Licha ya kusema anaziheshimu Morocco na Iran, Santos alisema ni ngumu kuziona timu hizo zikisonga mbele, ingawa zilikata tiketi ya kucheza fainali hizo za Urusi bila kufungwa katika michezo ya kufuzu.

“Ni kundi gumu, lakini Ureno wanatakiwa kukubali kuwa wanapewa nafasi. Hispania nao ni wazi wanapewa nafasi kama ambavyo nimekuwa nikisema,” alisema.

Akizungumzia ubora wa Morocco, Santos alisema: “(Katika mechi za kufuzu), Morocco wamefunga mabao huku wakiwa hawajaruhusu hata moja.

“Hiyo inaonesha ubora wa timu. Ina wachezaji waliowahi kucheza Ureno, (Mehdi) Benatia ambaye anakipiga Juventus na wana kocha mzuri,” alisema beki huyo wa zamani wa Ureno.

Pia, aliweza kuichambua Iran akisema: “Iran wao hii ni mara ya pili kucheza Kombe la Dunia, wana uzoefu na kocha wao ni mkongwe kwenye fainali hizi.”

Kwa mujibu wa ratiba iliyotoka, Morocco na Iran zitavaana Juni 15, siku ambayo pia Hispania na Ureno nazo zitakuwa zinatoana jasho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles