Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulika na Masuala ya Ukimwi (Unaids), limesema hadi kufikia Desemba 2016, watu milioni 36.7 walikuwa wanaishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU) duniani.
Akiwasilisha mada wakati wa kongamano la kisayansi kuhusu mwenendo wa Ukimwi nchini, Ofisa Mipango wa Unaids, Fredrick Macha, amesema kila siku kuna maambukizi mapya 5,000 kutoka kwa watu wazima na watoto duniani ambapo asilimia sita ya maambukizi hayo yanatoka katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Dk. Leonard Maboko, amesema matokeo ya utafiti wa viashiria vya Ukimwi nchini (2016/2017), yatatolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, Desemba Mosi.