24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

DC HAPI AAPA KUMNG’OA MDEE KAWE

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameahidi kumng’oa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Hapi alisema hakuna haja ya kuacha jimbo hilo la Kawe na majimbo mengine katika wilaya hiyo kuendelea kuwa chini ya upinzani kwa kuwa wananchi wana imani na CCM.

Kauli Hiyo aliitoa Dar es Salaam jana katika Kata ya Mbweni ambako CCM iliibuka na ushindi katika uchaguzi huo wa udiwani.

Alisema kutokana na matokeo ya uchaguzi kata ya Mbweni   Hashim Mbonde (CCM) aliibuka kidedea kwa kura 2049 dhidi ya Chadema  kura 1,093.

Alisema hizo ni salamu kwa Mdee kuwa mwaka 2020 atafute kazi nyingine na si ubunge katika jimbo hilo.

“CCM mpya haina makundi, wanaoshindwa na kushinda wote ni kitu kimoja na wale wanaokwepa falsafa za chama  watakaa pembeni,” alisema Hapi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni , Alord Maluma, alisema ushindi wa Mbonde  ni wa CCM na atahakikisha Kinondoni inarudisha uhusiano na uhusiano mwema wa wanachama na wannachi ili kukomboa kata, mitaa na majimbo.

Katika uchaguzi huo, CCM ilishinda kwa kupata kura 2049 Chadema 1093,  CUF 114 na SAU kura 12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles