23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

UTETEZI WA ‘SCORPION’WAKWAMA MAHAKAMANI

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

UTETEZI wa mshitakiwa, Salum Njwete maarufu ‘Scorpion’(35) anayekabiliwa na mashtaka mawili ya unyang’anyi na kujeruhi kwa kumtoboa macho Said Mrisho, umeendelea ‘kuota mbawa’ jana baada ya wakili wake kushindwa kufika mahakamani.

Kesi hiyo ambayo ipo kwenye hatua ya utetezi na iliyo mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule, iliahirishwa jana baada ya wakili huyo wa upande wa utetezi, Juma Nassoro kushindwa kufika mahakamani kwa sababu ya kuwa na kesi nyingine mahakama kuu.

Wakili wa Serikali, Ester Kyara akiwasilisha maombi hayo kwa niaba ya Wakili Mwandamizi wa Serikali Nassoro Katuga, aliiomba mahakama   kupanga tarehe nyingine kwa kuwa mshtakiwa ana haki ya kutoa utetezi mbele ya wakili wake.

“Kesi hii inakuja kwa ajili ya kuendelea na utetezi, lakini upande wa mashtaka tulikuwa tunaiomba mahakama yako tukufu kama itakupendeza ipange tarehe nyingine kwa kuwa wakili wa mshtakiwa ameshindwa kufika mahakamani kwa madai ya kuwa na kesi nyingine mahakama kuu.

“Hivyo kwa kutambua kuwa mtuhumiwa anayo haki ya kutoa ushahidi mbele ya wakili wake   tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya utetezi,” alidai Kyara.

Hakimu Haule alikubali maombi hayo na kupanga kesi hiyo kuendelea  Desemba 8, mwaka huu.

Novemba 20, mwaka huu wakati akianza kujitetea, ‘Scorpion’ katika sehemu ya utetezi wake alidai kuwa hahusiki na unyang’anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi, Mrisho.

Pia alidai yeye si mhalifu wala mwizi na hajawahi kupata kashfa zozote kama vile kugombana na watu, kuhusishwa na makosa ya jinai na kwamba jamii inamhitaji  kwa elimu anayoitoa kupitia sanaa za maigizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles