32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

KINANA, NAPE WAIBUKIA KAMPENI ZA UDIWANI ARUSHA

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameibuka katika kampeni wa udiwani mjini hapa na kudai ni ngumu kwa upinzani kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akihutubia katika Kata ya Makiba wilayani Arumeru mkoani Arusha leo kwenye kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo Samson Laizer, Kinana ambaye ameambatana na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, aliwataka kumchagua kiongozi atakayeshughulika na shida na si wapiga kelele.

“Kuna upepo ulivuma mwaka 2015 watu wakaaminishwa rafiki yangu yule atakuwa rais, bahati mbaya nyinyi mlifikiria nchi nzima imeishia Meru, mwaka 2020 tutakwenda kwenye uchaguzi mkuu tena, nchi hii naifahamu vyema nimezunguka yote uwezekano wa upinzani kushinda ni mgumu.

“Upepo ulishapita rais hakuwa, mawaziri hawana, hawakuunda Serikali wamebakia wenyewe wanasubiria 2020. Unadhani wananchi wataacha kumchagua Rais Dk. John Magufuli. Na yeye anajua kuna kura mwaka huo hivyo lazima ahakikishe anasimamia nidhamu serikalini, kujua mapato yote kwani na yeye anajua 2020 kuna kupigiwa kura,” amesema Kinana.

Aidha, amesema hakuja Makiba kupiga maneno bali kujua shida za wananchi ikiwamo maji, barabara umeme na zahanati ambapo amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuzitaja kero hizo ili kujua zitatatuliwa vipi kwa wananchi na kwamba uchaguzi huu si wa kishabiki ni wa kuondoa shida za wananchi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mtama CCM Nape Nnauye amesema, chama hicho kinaitaka Kata ya Makiba kwa gharama yoyote na kwamba atashangaa wananchi wa Kata hiyo wakimchagua kiongozi msindikizaji badala ya diwani anayetoka chama kilichounda Serikali.

“Nimekuja hapa Makiba, lazima tushinde uchaguzi tusipoteze muda kupiga ‘peoples’ hapa, Novemba 26, mwaka huu achaneni na maneno ya kufurahisha kampigieni kura mgombea wa CCM,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles