29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

UDSM YAJITAMBA KUZALISHA VIONGOZI LUKUKI

Profesa Rwekaza Mukandala

 

Na FARAJA MASINDE

UTAFITI uliofanywa na Taasisi ya Kimataifa ya Vyuo Vikuu vya Kati (4ICU) ya nchini Uingereza, Aprili, 2015, ulikitaja Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kushika nafasi ya 10 katika orodha ya vyuo vikuu 50 bora vilivyo maarufu barani Afrika.

Utafiti huo pia ulikitaja chuo hicho kuwa miongoni mwa vyuo vikuu vyenye idadi kubwa ya wanafunzi, walimu na masomo mengi. Katika utafiti huo, Chuo Kikuu cha Cape Town kilichopo nchini Afrika Kusini, kilishika nafasi ya kwanza.

Moja ya sifa ya utafiti huo ilikuwa ni namna ambavyo chuo kimekuwa msaada wa kutoa taarifa, kutafutwa kwenye mtandao wa Google, msaada wake kwa taifa na namna kinavyozungumzwa.

UDSM ni chuo cha kwanza nchini Tanzania, kinachopatikana katika Jiji la Dar es Salaam. Chuo hiki kilianzishwa mwaka wa 1970 baada ya kutengwa kwa Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki katika vyuo vikuu vitatu: Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda), Chuo Kikuu cha Nairobi (Kenya) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Licha ya kwamba UDSM kiliwahi kujizolea sifa kwa kuwa daraja la watu mashuhuli ndani na nje ya nchi wakiwamo, Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete ambaye kwasasa ndiye Mkuu wa chuo hicho, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Laurent-Désiré Kabila na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan, John Garang.

Wengine ni Mwanadipromasia wa Namibia, Joseph Obgeb Jimmy, Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Asha-Rose Migiro, Waziri Mkuu wa zamani nchini, Edward Lowassa na wengine wengi.

Bado chuo hicho kimeendelea kuzalisha wataalamu wengi ambao wamekuwa wakivunwa na Serikali kwa ajili ya kusaidia kusukuma maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Hili ni jambo la kujivunia kuona namna ambavyo chuo hiki kikongwe barani Afrika kilivyoendelea kuimarika katika eneo hili la kuandaa wataalamu katika sekta mbalimbali, ambao wamekuwa wakitumia ujuzi wao ndani ya nchi na hivyo kuifanya Tanzania kutohitaji kuajiri wataalamu wa nje ya nchi.

Hata hivyo ni wazi kuwa mafanikio ya kuandaliwa vyema kwa watalaamu hao yamekuwa yakichochewa kwa kiwango kikubwa na Serikali ambayo imekuwa ikifanya kila linalowezekana ili kuhakikasha kuwa inaweka mazingira rafiki kwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na chuo hicho kuweza kufikia malengo yao bila kuwapo kwa vikwazo visivyo vya lazima.

Mapema wiki hii, chuo hicho kimekamilisha mahafali yake ya 47 kwa wahitimu 7,089 wa ngazi mbalimbali, akiwamo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba aliyetunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Uchumi katika masuala ya fedha za kigeni na Rais mstaafu Kikwete.

Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, anatumia mahafali hayo kubainisha namna ambavyo chuo hicho kimekuwa na mchango mkubwa kwa Serikali kuhakikisha kinatoa wataalamu walio tayari kutumika serikalini wakati wowote.

Anasema chuo hicho kinajivunia mchango mkubwa ambao wanataaluma wake wa fani mbalimbali wameutoa katika kufanikisha jitihada zinazofanywa na Rais Dk. John Magufuli ili kuiweka Tanzania mbele kimaendeleo.

“Chuo kinamshukuru na kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa kuwatumia vyema wataalamu wetu wa ndani katika harakati za kuikomboa Tanznaia kiuchumi, hili ni njambo la kujivunia, kuona wanataaluma wetu wameendelea kuaminiwa na kuteuliwa katika nafasi nyeti kama uwaziri, ukatibu mkuu, unaibu katibu mkuu na ukurugenzi wa wizara mbalimbali.

Anasema chuo kimefurahi kuona Serikali ikiwaamini maprofesa na wataalamu mbalimbali wakiwamo, Profesa Palamagamba Kabudi ambaye awali alikuwa Mwanasheria Mkuu na Katibu wa Baraza la Chuo ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Machi mwaka huu.

“Wengine ni Naibu Makumu Mkuu wa chuo taaluma, Profesa Florens Luoga ambaye ameteuliwa kuwa Gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Oktoba mwaka huu, Profesa Joseph Buchweishaija aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji na Dk. Tulia Akson, Mbunge na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania.

“Teuzi zote hizi zinaonesha namna ambavyo UDSM kinavyotambulika kwa uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi nchini. Lakini pia haya yote kwa pamoja yanaendelea kutupa moyo na hamasa ya kuendelea kukisimamia chuo kwa nguvu zetu zote kuhakikisha kuwa kinaendelea kutoa elimu bora inayoambatana na maadili mazuri kwa wanafunzi wetu ili waweze kuwa viongozi wazuri wa baadaye,” anasema Profesa Mukandala.

Profesa Mukandala anasema licha ya chuo hicho kupata mafanikio, kumekuwa na kazi kubwa ambayo imekuwa ikifanywa kwa weledi na wanataaluma na wafanyakazi wa chuo hicho walioshiriki moja kwa moja katika uendeshaji wa programu mbalimbali zilizowalea vijana hao kitaaluma.

“Hivyo, tunasisitiza kuwa uwajibikaji, juhudi, maarifa na kujitoa kwa viongozi wa ngazi zote, wanataaluma wa fani mbalimbali na wafanyakazi wote wa UDSM, ndizo nguzo madhubuti zilizobeba mchakato mzima wa kuwafunza na kuwalea vijana hawa hadi kufikia walipo sasa.

“Dhamira yetu ni kuendelea kuandaa wataalamu wa kutosha ambao watakuwa tayari kulitumikia taifa lao wakato wowote wanapohitajika,” anasema Profesa Mukandala.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles