32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAGAZETI, MAJARIDA 100 YAPEWA LESENI

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

SERIKALI imetoa jumla ya leseni 109 za machapisho ya zamani na mapya ambapo kati ya hizo, leseni 85 ni ya zamani na mapya 24.

taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO  na Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abassi ilieleza kuwa, leseni hizo ni utekelezaji wa matakwa ya kifungu cha 5(e) cha Sheria mpya ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016.

Alisema mpaka sasa idara hiyo imekamilisha zoezi la awamu ya kwanza la utoaji wa leseni za uchapishaji wa magazeti na majarida  yaliyokua yamesajiliwa awali kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hiyo mpya.

“Hadi kufikia Oktoba 31, mwaka huu ambayo ni siku ya mwisho ya utoaji wa leseni za machapisho ya zamani na mapya, idara ya habari imetoa jumla ya leseni za machapisho 109, kati ya hizo 85 ya zamani na 24 mapya,” alisema Abbasi.

Alisema awali, Serikali iliwataka watu binafsi na taasisi kuchukua leseni hizo hadi ifikapo Oktoba 15, mwaka huu lakini waliongeza muda ili kutoa fursa kwa watu wasiokamilisha zoezi hilo hadi kufikia Oktoba 31.

Alisema taasisi, kampuni na watu binafsi walioshindwa kukamilisha zoezi hilo hawataruhusiwa kutoa machapisho yao bila ya kuwa na leseni hadi watakapoomba leseni upya.

Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 50 (2) (a) cha sheria ya Huduma za Habari 2016, ikithibitika kutenda kosa hilo, faini yake ni kati ya Sh milioni tano hadi 10, kifungo cha miaka mitatu hadi mitano au vyote kwa pamoja.

Alisema idara hiyo itaendelea kutoa huduma za kutoa leseni mpya kwa machapisho ya zamani na mapya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles