33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MWAKYEMBE ATAKA VYOMBO VYA HABARI KUTUMIA ALAMA ZA VIZIWI

Na Ashura Kazinja, Morogoro.


VYOMBO  vya habari, vimetakiwa kuajiri wakalimani wa kutafsiri lugha ya alama maalumu kwa viziwi ili kurahisisha mawasiliano na kuwapa viziwi haki ya kupata na kutoa habari.

Hayo yamebainishwa jana na Waziri wa Habari ,Utamaduni na Sanaa na Michezo, Dk. Harison Mwakyembe wakati wa kilele cha Wiki ya Vziiwi duniani iliyofanyika mkoani hapa.

Alivitaka vyombo vyote yva habari kuwa na wakalimani wa lugha ya alama waliopitia Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ili kuepuka kuajiri wataalamu wasiokuwa na sifa.

Alisema kila chombo cha habari, kinatakiwa kuajiri wakalimani sita muda utakapofika ingawa kwa sasa wataanza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa wataalamu wanne na kisha kuingia katika vyombo vingine  vya habari vinavyomilikiwa na watu binafsi.

“vyombo vyote vya habari vinatakiwa kuwa na wakalimani wa lugha ya alama ambao wamepitia BAKITA, tutaanza na taarifa zote za habari halafu polepole tutaenda katika vipindi vingine, ili kufanya vizuri lazima wakalimani wawe sita kila chombo, lakini kwa kuanza na tbc wanne wanatosha na baadae tv zingine zitafata” alisema mwakyembe.

Naye mwakilishi wa walemavu na Mbunge Viti Maalumu Stella Ikupa, aliiomba Serikali kuiingiza kwenye mitaala ya shule za msingi na sekondari lugha ya alama ili jamii iweze kujifunza na kuwasiliana kwa urahisi.

Alisema lugha hiyo,ni vyema ikafundishwa kwa wafanyakazi wa taasisi zote ikiwemo jeshi la polisi, madaktari na watoa huduma mbalimbali ili kurahisisha viziwi  kupata haki zao sambamba na huduma mbalimbali katika jamii kwa urahisi kutokana na jamii kuwaelewa wanachoongea.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Chama cha Viziwi Tanzania( CHAVITA) Mkoa wa Morogoro, Hodavia Lugakingira alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo ya elimu kutokana na kutokuwepo kwa vyuo vya viziwi na kuwafanya viziwi wengi kushindwa kupata elimu ya juu na kuishia elimu ya sekondari.

Alisema kumekuwa na ugumu kwa viziwi kupata huduma muhimu kama ya matibabu kutokana na wauguzi na madaktari kutoaelewa wanasumbuliwa na maradhi gani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles