25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

BELLA KUWASHA MOTO ‘NYERERE DAY’

Na JESSCA NANGAWE-DAR ES SALAAM

MFAMLE wa muziki wa dansi nchini, Christian Bella, anatarajia kufanya shoo ya aina yake usiku wa Oktoba 14,  sambamba na kuenzi kifo cha Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza na MTANZANIA, mwandaaji wa shoo hiyo, Victoria Chilala, alisema shoo hiyo itakuwa maalumu kwa ajili ya siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu, ambapo mbali ya msanii huyo pia kutakuwa na wasanii wengine watakaotumbuiza.

“Tunatarajia shoo ya aina yake ambayo itaongozwa na mfalme wa muziki wa dansi hapa nchini Bella, hii ni mahususi kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, sambamba na kutoa burudani kwa wakazi wa Sinza,” alisema Victoria.

Alisema shoo hiyo itafanyika katika ukumbi wa De Francie uliopo Sinza, huku wasanii wengine watanaotarajiwa kutumbuiza, wakitarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Christian Bella kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Punguza Mikogo’, ambacho kinafanya vyema kwenye stesheni mbalimbali za redio hapa nchini na nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles