23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

NIKOTINI KWENYE ASALI HAINA MADHARA 

Na MWANDISHI WETU


WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetoa ripoti ya utafiti wa asali yenye chembechembe za kemikali  ya nikotini iliyofanyiwa majaribio na kuonyesha kwamba haina madhara kwa binadamu.

Akizungumza jana, Meneja Mawasiliano wa TFS, Glory Mziray alisema wamekuwa wakikusanya sampuli kila baada ya miaka miwili  kutoka kwa wafugaji nyuki na kuzipeleka kwenye  maabara za kimataifa.

Alisema  mara zote  zimekutwa   na ubora wa hali ya juu unaokidhi masoko ya taifa na mataifa.

Mziray alitaja utafiti uliofanyika mara mbili mwaka 2016 kuwa  lengo lilikuwa ni kuainisha madhara ya ufugaji nyuki kwenye maeneo yanayolima tumbaku.

Aliyataja maeneo ambayo yaliyofanyiwa utafiti huo kuwa  ni mikoa ya Tabora na Kigoma.

Mziray alisema utafiti huo ulionyesha  kuwa kiwango cha nikotini kinachopatikana  kwenye asali iliyochavushwa katika mikoa inayolima tumbaku ni sawa na nikotini inayopatikana kwenye asali  ilivyochavushwa na mimea mingine.

Alisema watumiaji wa asali wamekuwa wakihukumu uwepo wa  nikotini   kwenye asali kwa kuangalia rangi,uchungu lakini asali ya Tanzania inatengenezwa kwa mchanganyiko wa maua ya mimea mbalimbali  jambo ambalo linathibitishwa si nikotini peke yake ndiyo inasababisha uchungu bali mimea mingine kama vile muarobaini.

Mziray amewataka watumiaji wa asali kuendelea kuitumia kwa vile  ni chakula cha asili kinachotengenezwa kwa mchanganyiko wa mimea mbalimbali.

Alisema  asali ni mchanganyiko wa maji, sukari (fruktosi, glukosi, sakrosi) madini   na vitamin ambayo inaleta afya kwenye mwili wa binadamu na si vinginevyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles