31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

UKEKETAJI BADO WALITESA TAIFA

Na ASHA BANI


WANAHARAKATI, wanasheria na taasisi  mbalimbali za Serikali zimesema tatizo la ukeketaji bado kubwa nchini.

Dk. Natujwa Mvungi kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Wanasheria Tanzania alikuwa akizungumza hayo   Dar es Salaam jana   baada ya mkutano wa wadau hao.

Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kupinga ukeketaji nchini.

Alisema kuna haja ya kubadilisha baadhi ya vifungu vya sheria ambavyo vitamsimamia mwanamke na mtoto wa kike katika kupinga ukeketaji.

Dk. Mvungi alisema kuna sheria mbalimbali zinazungumzia  ukeketaji lakini zinaangalia mtoto wa kike chini ya umri wa miaka 18 na si zaidi ya hapo.

‘’Kuna watoto walio chini ya miaka 18 na hata wanawake waliozidi umri huo wote wanaathirika kutokana na mila hizo hivyo ni vema kukafanyika mabadiliko sheria  iwe kwa wanawake na  watoto,” alisema.

Alisema  suala la ukeketaji katika katiba ya mwaka 2011 ya  Kenya na ile ya 2010 Uganda limewekwa na linafanya kazi kwa watoto na wanawake.

Pia alisema katika nchi za Afrika ya Mashariki ni ajenda  kubwa kwa mwaka 2017 kupinga   ukeketaji kwa mtoto wa kike na mwanamke.

Alisema ni jambo la kushangaza katika Tanzania hakuna kipengele kwenye Katiba kinachozungumzia  suala la kupinga ukeketaji.

Alisema sheria ya watoto ya mwaka 2009 na ile ya makosa ya jinai ya mwaka  2002 imekuwa ikikinzana kwa baadhi ya adhabu zake jambo ambalo si zuri.

“Ombi letu kwa wadau na kwa serikali ni kwamba sheria hizo zisipingane maana sheria ya watoto  inasema kwamba ukikutwa na kosa la ukeketaji ni kifungo cha miaka 15 au  faini   Sh milioni mbili   huku sheria ya jinai   faini yake haizidi Sh 300,000,’’alisema.

Wakili kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Naemy Silayo alisema hadi sasa   utafiti  unaonyesha  mikoa inayoongoza kwa ukeketaji  ni   Dodoma asilimia 47. Arusha asilimia 41, Singida asilimia 31 na Mara asilimia 32.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles