26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

GIGY MONEY AIMBE TU LAKINI AJUE KUNA RUBBY

Na RAMADHANI MASENGA

KATIKA dunia ya utandawazi hutakiwi kuwa na misimamo isiyobadilika( Rigid). Mbali na kuamini sana mambo fulani, kanuni fulani ama hisia fulani ila pia unatakiwa kujua wakati unataka nini na kitu gani ukubali ama ukatae.

Katika dunia ya muziki kuna wasanii wa aina tatu. Kwanza kuna wasanii wakali. Pili kuna wasanii promo. Tatu kuna wasanii wanaojitahidi. Habari njema ni kwamba hawa wote ni muhimu kutokana na mahitaji ya wakati.

Wasanii wakali wanajulikana. Katika kundi hilo wapo wakina Young Killer, Harmonize, Msami na kina Diamond. Wasanii wanaojitahidi ni kama wakina Snura, Shilole na Hemed Suleiman. Wasanii promo wako wengi mno, miongoni mwao wako akina Gigy Money na Lulu Diva. Hapa japo kila mmoja ana uwezo wake na umahiri wake ila pia wamezidiana sana.

Mfano. Mbali na Msodoki kuwa msanii mkali na mwenye mashairi adimu ila amezidiwa sana na Hemed Suleiman namna ya kujiweka kisanii. Hapa sizungumzi muonekano halisi( natural physical appearance). Nazungumzia namna anavyojiweka ili popote awapo ama lolote analofanya liwe habari na kuweza kuweka jina lake juu zaidi. Hili msodoki mbali na kipaji kikali. Akili iliyotulia ila kitu hiki hana.

Hata Rubby. Mbali na kuonekana na vituko fulani ila kuna kitu anakosa. Anakosa namna ya kujiwekea ushawishi binafsi kama msanii. Mbali na kuwa mbabaishji katika sanaa ila Gigy Money akituliza akili ana uwezo wa kuwa na kitu hiki na kukimbiza sana Rubby.

Kuna mambo watu wanashindwa kuelewa kuhusu ukali wa Diamond Plutnumz. Mbali na kuwa na kipaji kikali ila Diamond ameweza kujitengeneza na kuwa msanii bidhaa. Hiki wasanii wengi wakali hawana. Barnaba hana, Ali Kiba hana, Amin hana na wengine pia hawana. Ndiyo maana mpaka sasa kuna baadhi ukiwaambia Diamond ni msanii mkali Afrika mashariki na kati wanashindwa kuelewa.

Wanashindwa kuelewa kwa sababu kwao sanaa ama muziki unaishia katika sauti na na mashairi pekee. Hapana. Katika dunia ya sasa ya utandawazi sanaa ni zaidi ya hapo. Sanaa ni jumla ya unavyoishi wewe na kutengeneza jina lako.

Kwa zaidi ya miaka nane sasa jina la Diamond liko juu sio kwa sababu ya nyimbo zake tu. Ni zaidi ya hapo. Hata namna anavyoachia nyimbo zake ziko katika hali fulani ya utata ambao inafanya wapenzi wa muziki wajawe na shauku kabla.

Nilikuwa namsikiliza msanii fulani akijisifia maisha yake ya kukaa maskani kama zamani kabla hajawa msanii. Alisema yeye bado hajabadili maisha na hategemei kubadili misha yake. Kwake kufanya hivyo ndio ubinadamu. Ndiyo uungwana. Na ndiyo utanzania.

Asichokijua ni kwamba ili thamani na hadhi yake ionekane juu ni lazima abadili mfumo wake wa maisha. Ni lazima aifanye jamii yake imuone yeye sio wa kawaida tena kama ilivyo kuwa manzo. Mbinu hii ndiyo inatumiwa na wasanii wengi wenye kujua mitikasi na mizungu ya biashara ya burudani. Hii ndiyo mbinu inayofanya Diamond kila siku aonekane mpya katika macho ya mashabiki wake na kufanya kampuni kubwa za biashara zimkimbilie.

Angalia watu kama kina 20% na Afande Sele. Mbali na majina yao makubwa. Mbali na nyakati fulani kuweza kusimamisha nchi katika matembezi yao. Ila nini kiliwakwamisha kuwa wasanii bidhaa? Wasanii wenye kubabaikiwa na wadau na makapuni makubwa kwa ajili ya dili za matangazo? Ni usela wao uliokithiri uliofanya wajichanganye hovyo na kuonekana watu wa kawaida sana mbele ya macho ya wapenzi wa muziki.

Gigy Money pamoja na ya hovyo yake usishangae akawa msanii mkubwa kuliko Ruby. Nasema usishangae. Kuna uchawi anaujua wengine hawaujui. Hata hii nyimbo yake mpya inayokwenda la Papa. Uchaguzi wa hilo jina uliona mbali kuliko kawaida. Alikua akitaka watu wapate shauku baada ya kusikia jina la nyimbo yake ili waweze kuisaka. Akili hii hata Ali Kiba mbali na uwezo wake mkubwa katika kuimba na kuandika ila hana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles