26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya Bunge yamfukuza Magufuli

magufuliPatricia Kimelemeta Jonas Mushi, Dar es Salaam

KAMATI ya Bunge ya Miundombinu, imemfukuza Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli baada ya kushindwa kutoa maelezo ya namna Serikali itakavyoweza kulipa madeni ya wakandarasi yanayofikia Sh trilioni moja.

Dk. Magufuli alikumbana na kibano hicho cha kamati hiyo ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wake Peter Serukamba, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kamati hiyo kiliambia MTANZANIA jana kuwa wakati wa kikao hicho Waziri Magufuli aliwasilisha mapendekezao ya bajeti ya wizara yake lakini wajumbe waligeuka mbogo.

Wajumbe walianza kumbana kwa maswali magumu hasa baada ya kutoonekana kwa kifungu kinachoainisha mkakati wa ulipaji wa madeni ya wakandarasi wa barabara.

Kutokana na hali hiyo, waziri huyo alitakiwa na wajumbe wa kamati hiyo kumwita Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenda mbele ya kamati hiyo ili aweze kutoa ufafanuzi wa namna Serikali itakavyolipa deni hilo.

“Tumeshindwa kujadili na kupitia hesabu za Wizara ya Ujenzi kwa sababu bajeti yao haioneshi namna ya kulipa deni la Sh trilioni moja. Kutokana na hali hiyo kamati kwa kauli moja ikakubaliana ni vema waziri aje mbele ya kamati na waziri mkuu kama kiongozi wa Serikali kwani anaweza kutoa dira nzuri kuliko kukaa kimya,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba, ili aweze kutoa ufafanuzi hakupatikana katika eneo la ofisi ndogo za Bunge na wala katika simu.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Zarina Madabida alipoulizwa juu ya uamuzi huo, alikiri kamati hiyo kukutana na waziri Magufuli na kueleza kuwa kamati ilikubaliana kumsaidia kwa kumwita waziri mkuu mbele ya kamati kama njia ya kunusuru utekelezaji wa miradi ya barabara nchini.

“Lengo letu ni kumsaidia Magufuli kujua namna ya ulipaji wa deni hilo, jambo ambalo linaweza kurahisisha upitishaji wa bajeti ya wizara yake,”alisema Zarina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles