25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MUSEVENI ASHEREHEKEA MIAKA 70 YA UBATIZO

MBARARA, UGANDA

RAIS Yoweri Museveni amesherehekea miaka 70 katika Kanisa la Uganda la Mtakatifu Luka, huko Rwampara wilayani Mbarara.

Hilo ni kanisa ambalo Museveni alibatizwa Agosti 3, 1947.

Alisema alibatizwa wakati alipokuwa na miaka miwili na miezi 11. Kwa mujibu wa kumbukumbu za kanisa hilo, ubatizo wa Museveni ni namba 3769.

Alibatizwa siku moja na wazazi wake Amos Kaguta na Esteri Kokundeka, ambao wote ni marehemu.

Familia hiyo ilibatizwa kuingia Ukristo, hivyo wazazi wake wakaoana upya kwa ndoa ya Kikristo.

Mchungaji aliyewabatiza, Eric Sabiiti baadaye akaja kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Uganda.

“Nataka kumshukuru Mungu kwa miaka 70 niliyoishi tangu nibatizwe, kwa sababu ni miaka mingi na bado nina nguvu,” alisema Museveni katika hafla ya kutoa shukrani.

Aidha katika hafla hiyo, Museveni alifichua kuwa alizaliwa Septemba 1944 na kwamba atakuwa na umri wa miaka 73 mwezi ujao.

Hata hivyo, alisema hana cheti chake cha kuzaliwa kwa sababu hakuweza kukiona katika Hospitali ya Mbarara, ambako alizaliwa.

Tukio lake hilo la kusherehekea miaka 70 ya ubatizo na kauli ya kutimiza miaka 73 mwezi ujao, inakuja wakati ambao kuna harakati zisizo rasmi za kutaka kubadili Ibara 102 ya Katiba, kuondoa ukomo umri wa urais.

Hilo linamaanisha kuwa iwapo Katiba haitabadilishwa, Rais Museveni hataweza kuwania tena urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2021 kwa sababu atakuwa amepita miaka 75 ya ukomo unaoruhusiwa kikatiba.

“Nilizaliwa Hospitali ya Mbarara  wakati ikiwa katika ofisi za halmashauri kabla ya kuhamishwa Chuo Kikuu cha Mbarara. Lakini wakati nilipoenda kutafuta cheti changu cha kuzaliwa, sikuweza kukipata. Wakati nilipoanza kuuliza wazee, waliniambia nilizaliwa Septemba 1944,” alisema Museveni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles