26.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

NBS YAONYA UTAFITI WA KAMPUNI YA GEOPOLL

CECILIA NGONYANI (TUDARCO) Na TUNU NASSOR

  • DAR ES SALAAM

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imeionya Kampuni ya Geopoll kwa kutoa takwimu ambazo hazijafuata taratibu katika ukusanyaji wake na hivyo kuleta mkanganyiko katika jamii.

Hivi karibuni kampuni hiyo yenye Ofisi ya Kanda ya Afrika jijini Nairobi, Kenya ilitoa takwimu kwa njia ya mitandao ya kijamii zinazoonyesha taarifa za idadi ya watazamaji wa televisheni na wasikilizaji wa redio nchini kwa muda wa miezi mitatu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa, alisema takwimu zilizotolewa na kampuni hiyo hazikukidhi vigezo kwa mujibu wa sheria ya takwimu ya mwaka 2015.

Alisema kifungu cha 20 cha Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, kinazitaka taasisi au mtu binafsi kufuata misingi ya utoaji takwimu rasmi ikiwa ni pamoja na mfumo wa ukusanyaji na utolewaji wake kuratibiwa na NBS.

“Kwa mantiki hiyo, takwimu za Geopoll hazikukidhi vigezo vinavyotolewa NBS, hivyo hatuzitambui kuwa ni takwimu rasmi na haziwezi kutumika katika kupanga mipango ya maendeleo ya nchi,” alisema Dk. Albina.

Alisema NBS inaitaka Kampuni ya Geopoll kufuata taratibu zilizoainishwa katika sheria ya takwimu kinyume cha hapo takwimu zao zinapotosha jamii na kuleta mkanganyiko kwa wadau wa habari na kuathiri mahusiano ya kiutendaji baina ya vyombo vya habari hapa nchini.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa, aliwataka waandishi wa habari kutokutumia takwimu hizo hadi wizara kwa kushirikiana na NBS itakapotoa nyingine zitakazoandaliwa kwa kuwashirikisha wadau wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles