26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

UHURU: KUNA KENYA BAADA YA UCHAGUZI

Mgombea urais wa Chama cha Jubilee nchini Kenya, Uhuru Kenyatta amewataka  Wakenya kutoruhusu uchaguzi kuwagawa kwa sababu Kenya itaendelea kuwepo hata baada ya uchaguzi.

Akizungumza baada ya kupiga kura Kaunti ya Gitundu, Kenyatta amesema kulikuwa na kampeni za amani na anaamini Wakenya wana hamu ya kuendelea na amani hiyo baada ya uchaguzi.

“Uchaguzi usitugawe sisi ni ndugu hata bila uchaguzi na baada ya uchaguzi, nawaambia amani, amani, amani… kila Mkenya apige kura aende nyumbani asubiri matokeo tutakuwa na Kenya baada ya uchaguzi na tutaendelea kuwa ndugu, dada, kaka na jirani hata baada ya uchaguzi.

“Nimetumia saa mbili katika foleni ya kupiga kura naona amani imetawala, fujo na vurugu zinaharibu Kenya yetu,” amesema.

Aidha, amesema endapo mpinzani wake atashinda katika uchaguzi huo ataheshimu maamuzi ya Wakenya na atashirikiana naye kuongoza pamoja kuipeleka Kenya mbele kwa maslahi na faida ya Wakenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles