25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mimba, kivuko vyamkosesha usingizi DC

Na BENJAMIN MASESE

-NANSIO

MKUU wa Wilaya ya Ukerewe, Estomih Chang’ah, amesema hali ya usalama wa wilaya hiyo si shwari kutokana na   viasharia ambavyo vinaweza kusababisha maafa muda wowote.

Alimwomba Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula kulifikisha suala hilo sehemu husika.

Chang’ah alisema moja ya kiasharia cha kutokuwapo  usalama wa raia ni kivuko cha MV Nyerere ambacho hufanya safari zake kati ya Ukara na Bugorola

Alisema kivuko hicho kimekuwa kikizua hofu mara kwa mara kutokana na kuharibikia katikati ya ziwa.

“Kwa kuwa wilaya hii ipo kisiwani na baadhi ya wakazi wa Ukerewe   wanaishi katika visiwa vidogo vidogo, ninaweza kusema hali si shwari kwa baadhi ya wananchi hasa wanaosafiri au kusihi Ukara na Bugorola.

“Naomba suala hili ulifikishe kwa wizara husika ili lifanyiwe kazi kwa uzito wake,” alisema.

Alisema jambo la pili ambalo si zuri  ni vitendo vya watoto wa shule kupewa ujauzito.

“Hapa Ukerewe mimba si za kuuliza.  Kibaya zaidi tunapofuatilia ipo tabia ya wazazi kushirikiana na watuhumiwa na kuyamaliza huko huko.

“Tunashindwa kupata ushirikiano   kumkamata aliyempa mimba mtoto, isitoshe na hata mwanafunzi anakuwa hayupo tayari kumtaja.

“Jambo hilo ni kubwa kwa kiasi chake ingawa vyombo vya dola vinapambana nalo… tunashindwa kufikia malengo ambayo tunayakusudia  yaani Ukerewe wanazaliana kweli kweli,” alisema.

Naye  Waziri Mabula alisema suala la kivuko, katika bajeti ya 2017/2018, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imekitengea fedha na aliahidi kulifikisha kwa waziri husika.

Kuhusu mimba, alisema kwa mujibu wa sheria, mtuhumiwa anapaswa kwenda jela miaka 30.

Aliomba uwepoa mpango wa kuangalia kufanya maboresho ya kuwahusisha wazazi wa wanafunzi ambao wanashindwa kutoa ushirikiano ili nao wajumuishwe katika adhabu ya miaka 30 jela.

“Kuhusu uvuvi haramu, hili suala lipo katika Wilaya ya Ukerewe, Musoma na Ilemela, sasa ninachoomba ifanyike operesheni ya pamoja ambayo itahusisha vyombo vyote.

“Maana tukifanya hapa Ukerewe watakimbilia kule Musoma au Ilemela, sasa tujipange ili msako ufanyike kwa pamoja katika wilaya zote,” alisema.

Wakati huohuo, Naibu Waziri amemfuta cheo, Ofisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe,  Eliah Mtakama  akidaiwa kuwa mzembe kazini na kushindwa kutimiza majukumu yake kwa  miaka 14.

Vilevile, alimfuta cheo, Ofisa Ardhi Msaidizi wa Wilaya hiyo, Samwel Msungu, kabla ya kurejeshewa tena  baada ya kuwasilisha nyaraka  alizozitoa  wizarani akielezea changamoto ambazo zilimfanya kutotimiza majukumu yake ipasavyo ya kuingiza takwimu katika mfumo maalumu wa  utambuzi wa wamiliki wa viwanja na ulipaji kodi kwa miaka miwili mfululizo.

Mabula alichukua hatua hiyo baada ya Mtakama kuwasilisha taarifa ya idara ya ardhi katika wilaya hiyo  huku ikiwa na upungufu mkubwa ambao ulisababisha kuongezeka migogoro  kati ya wananchi na serikali, taasisi za dini na mashirika binafsi na hakuna jitihada zilizowekwa kutatua kero hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles