24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wahisani watoa bil. 100/- ujenzi barabara Kidatu-Ifakara

Na Tobias Nsungwe – Dar es Salaam

WIZARA ya Fedha na Mipango imetiliana saini na kampuni ya ujenzi wa barabara ya Reynolds  kw ajili ya ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara mkoani Morogoro.

Barabara ya kilometa 67 itajengwa kwa kiwango cha lami   kwa gharama ya Sh bilioni 101 kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU), Marekani na Uingereza.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango, ilisema mkataba huo ulisainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaaban  na  Benjamin Arbit ambaye ni mkandarasi kutoka Kampuni ya Reynolds.

Taarifa hiyo imesema ujenzi wa barabara hiyo utahusisha ujenzi wa daraja katika Mto Ruaha  na  itasaidia wakulima wadogo kupitia Mpango wa Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) kaika Bonde la Mto Kilombero ambao wataweza kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao.

“Kuimarika kwa kipande hiki cha barabara kutaongeza uzalishaji wa nafaka na bidhaa nyingine hatimaye kupunguza gharama za chakula na umasikini wa wananchi.

“Ujenzi wa miundombinu unalenga kuchochea maendeleo ya kilimo cha  biashara kwa kuwa utasaidia kuwakutanisha   wafanyabiashara na wakulima,” alisema Amina.

Alisema barabara ya Kidatu hadi Ifakara ndiyo inayounganisha wilaya za Kilombero na Ulanga na ni barabara kuu inayokwenda Zambia, Malawi na   Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Balozi wa EU hapa nchini, Roeland van de Geer, aliahidi kuwa EU  UKAID na USAID, zitaendelea kushirikiana kwa kiwango cha juu na Serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya ujenzi na miundombinu kwa ujumla.

Alisema  atahakikisha EU inachangia katika kupata soko la uhakika la mazao ya kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles