25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri kujenga hospitali ya kisasa

Na SEIF TAKAZA

-SINGIDA

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida inatarajia kujenga hospitali ya wilaya ya kisasa kwa nguvu za wananchi na wadau wa maendeleo   ndani na nje ya wilaya hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,  Godfrey Sanga alisema hayo katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilichofanyika mjini Nduguti juzi.

Alisema ujenzi huo unahitaji ekari 30 hadi 50 kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma zote muhimu za rufaa kutoka zahanati na vituo vya afya.

“Sh bilioni 4.5 zinahitajika kugharimia hospitali hiyo ya kisasa ambayo ujenzi utafanyika kwa awamu tatu kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu.

“Awamu ya kwanza zinahitajika Sh bilioni 1.5, ambazo zitapatikana kwa kuchangiwa na wananchi kila kijiji.

“Nyingine ni harambee ya ujenzi wa hospitali, michango ya wadau wa maendeleo, watumishi wa halmashauri na serikali kuu na mikopo isiyo na riba,” alisema.

Alisema awamu pili inahitaji Sh bilioni 1.8 na ya tatu Sh bilioni 1.14 na mchakato huo unatarajiwa kukamilika kwa awamu ya kwanza Juni 30 mwaka 2019 na kakamilika   mwaka 2021.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, James Mkwega alisema katika mchakato huu wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkalama ukiwapo ushirikano thabiti inaweza kujengwa hata kabla ya mwaka 2021.

“Tuhakikishe tunatumia wataalamu wetu vizuri kuanzia wilaya, mkoa na Wizara ya Afya kuhakikisha wanasimamia vizuri kazi ya ujenzi wa hospitali yetu.

“Pia tuwaarifu wadau wetu wa ndani na nje ya mkoa wetu na walioko nje ya nchi kutusaidia ujenzi wa hospitali yetu,’’ alisema Mkwega.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles