29.9 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Magufuli abaini ubadhirifu ujenzi wa barabara

Waziri John Magufuli
Waziri John Magufuli

Na Charles Mseti, Mwanza

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amegundua ubadhirifu wa fedha zaidi ya Sh bilioni tano katika ujenzi wa barabara ya Usagara kwenda Kisesa mkoani Mwanza.

Ubadhirifu huo ameugundua jana wakati akikagua mradi wa barabara hiyo inayojengwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mwanza.

Alisema ucheleweshwaji wa ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita tano zilizotarajiwa kukamilika Agosti, mwaka huu umetokana na ubadhirifu huo.

Alisema kitendo hicho kimetokana na kampuni hiyo kupitisha barabara eneo ambalo ni kinyume na makubaliano ya awali ya mkataba wao na Serikali.

“Kama tukiendekeza tabia za namna hii za kupenda vitu ambavyo vina manufaa kwenu na kutaka kupitisha barabara eneo la Halmashauri ya Magu kinyume na makubaliano ambayo tulipatana awali hatutafika mbali.

“Kuna barabara nyingi ambazo zinatakiwa kujengwa na Serikali, lakini watu wachache wanataka kurudisha juhudi zilizopo na sasa hatutakubaliana na vitendo vya namna hiyo, nataka barabara ipite ile sehemu ya zamani.

“Hamuwezi kuacha eneo la zamani kwa kuwa kuna baadhi ya watu wanataka kujenga vitega uchumi vyao na mkachelewesha mahitaji ya walio wengi na sisi Serikali tunataka wananchi wapate barabara ya lami,” alisema Dk. Magufuli.

Kwa upande wake, Mhandisi wa TANROADS Mkoa wa Mwanza, Elias Boniphace, alisema ujenzi wa barabara hiyo umechelewa kutokana na ucheleweshwaji wa malipo ya fedha kwa kuwa hadi sasa kiasi kilicholipwa ni zaidi ya Sh milioni 173 lakini mkandarasi anadai zaidi ya Sh bilioni tatu.

“Ujenzi wa barabara hii yenye urefu wa kilomita 16.8 kwa kiwango cha lami na ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 67.95 na makalavati kumi na nne ni zaidi ya shilingi bilioni 17,” alisema Elias.

Alisema ucheleweshwaji wa malipo hayo kunasababisha mradi huo kuchelewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles