27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Makalla atatua kero jimboni kwake

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

NAIBU

Amos Makalla
Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero (CCM), Amos Makalla

, ameendelea kutatua kero za wananchi wake kwa kutoa misaada mbalimbali.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati akikabidhi misaada hiyo yenye thamani ya Sh milioni tano, alisema hiyo ni utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa kata hizo ili kurahisisha maendeleo na huduma za kijamii.

Misaada hiyo aliitoa katika kata ya Hembeti, Pemba na Kibati ikiwa na lengo la kuharakisha maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo.

Miongoni mwa taasisi zilizonufaika na misaada hiyo ni pamoja na shule tatu za awali zilizopo Kata ya Pemba na ujenzi wa ofisi ya kata hiyo, taasisi za dini na vikundi mbalimbali vya wajasiriamali katika kata ya Hembeti na Kibati.

Alipozitembelea kata hizo, alisema wananchi walimkabidhi kero hizo na kuahidi kuzifanyia kazi haraka ili kuleta chachu ya maendeleo yao.

Aliwahakikishia wananchi wa Turiani na Mvomero kuwa Serikali itaendelea kutatua kero mbalimbali za mawasiliano, barabara, umeme na huduma za maji.

Alisema katika mwaka wa fedha wa 2014/2015, tayari Serikali imetenga fedha za kumaliza miradi iliyokuwa haijakamilika na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kuvuta subira.

Alitolea mfano wa barabara ya Mvomero-Ndore na Kibati kuwa uboreshaji wake ikiwa pamoja na kuitanua barabara hiyo unaanza muda wowote kuanzia sasa ili kurahisisha usafiri wa uhakika katika kipindi cha mwaka mzima.

Kuhusu mawasiliano ya simu katika kata ya Hembeti na Kibati, alisema tayari Serikali imeshamuhakikishia ujenzi wa mnara huo utakaofanywa na Kampuni ya Zantel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles