26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

JK kuzindua kitabu cha muungano leo

Rais Jakaya KikweteRuth Mnkeni na Veronica Romwald, Dar es Salaam
RAIS Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu kinachoelezea historia ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, mwandishi wa kitabu hicho kilichopewa jina la ‘Photographic Journey’, Javed Jafferji alisema lengo la kuaandaa kitabu hicho ni kuonesha matukio muhimu ambayo Tanzania imepitia tangu nchi hizo zilipoungana mwaka 1964.
“Tumepitia mambo mengi, bado tumeendelea kudumisha ushirikiano wetu, tukaona ipo haja ya kuyaweka kwa pamoja ndani ya kitabu ili kuwasaidia wale ambao hawajui waweze kuyajua,” alisema.
Alisema kitabu hicho ambacho kina kurasa 444, kinaelezea historia ya viongozi mbalimbali waliopita, Azimio la Arusha, ujenzi wa reli ya TAZARA na vita ya Kagera.
“Kitabu hiki ni cha kwanza na kina baraka zote za marais wetu wa pande zote mbili, kitasaidia watu kufahamu historia mbalimbali ndani ya Tanzania pia kitaweza kutumika mashuleni pamoja na kuutangaza utalii wa ndani,”alisema Jafferji.
Kwa upande wake, mwandishi na mhariri wa kitabu hicho, Simai Said alisema upo umuhimu wa kuweka kumbukumbu vizuri kwa ajili ya manufaa ya kizazi kijacho.
“Katika uandaaji wa kitabu hiki tumetumia picha mbalimbali ambazo zinaelezea matukio tofauti tofauti yaliyotokea ndani ya kipindi cha kati ya mwaka 1964 hadi 2014 lakini tulitumia muda wa zaidi ya miezi 17 kuzipata,”alisema Javed.
Alisema uzinduzi huo utahudhuriwa na watu mbalimbali ambao wameandikwa ndani ya kitabu hicho ikiwa ni sehemu ya kuutambua mchango wao walioutoa kwa Taifa, akiwamo Mtanzania wa kwanza na mwafrika wa pili kupanda mlima Evarest ambao ni mrefu kuliko yote duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles