29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

BEN KAZORA: TUNAISHI MAREKANI LAKINI FIKRA ZETU ZIPO TANZANIA

Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania dallas (kushoto), Benedict kazora akiwa na Naibu Meya wa Mji wa Dallas Erik Wilson.

 

 

APRILI 29, mwaka huu Watanzania wanaoishi katika Mji wa Dallas  nchini Marekani waliandaa tukio muhimu la kihistoria kwa kukumbuka Utanzania wao na kueleza kwa Wamarekani yale mambo mazuri yenye tija yaliyopo Tanzania kwa ajili ya kuitangaza  nchi yao Mama. Benedict Kazora Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania walioko Dallas, alifanya mahojiano kwa njia ya mtandao na Mwandishi wetu SARAH MOSSI na yafuatayo ni mahojiano hayo

MTANZANIA:  Kwanini mmeamua kuwa na  Tanzania Day?

KAZORA:  Baada ya kukaa kwa kipindi kirefu hapa Marekani kila mmoja wetu akiingia kwa njia iwe za masomo au kutafuta maisha na kupitia changamoto mbalimbali za ugenini na baada ya kujiona sasa tumeweza kukaa sawa kimaisha, kujielimisha na kusurvive na kuwa stable kimaisha na kuanza kuona changamoto zetu zimeanza kubadilika. Yale maswali tuliyoanza kujiuliza mwanzoni na kuanza kukomaa yanabadilika na kuanza kujiuliza, Mimi ni Mtanzania nimechangia nini katika maendeleo ya nchi yangu, nimechangia vipi katika elimu ya nchiyangu, afya, utalii na sehemu tofauti. Kwa sababu kumbuka ni baraka kuwa hapa.

Mimi Mtanzania ninayeishi Marekani ni rahisi kumpigia simu Seneta wangu na kuitetea nchi yangu nikiwa huku. Kwahiyo Ukiwa huku wewe ni balozi was kuiuza nchi yetu. Nchi yetu ina mambo mengi sana ya sifa hasa ukiangalia kwenye uongozi wa Tanzania katika Bara la Afrika, kiuchumi, kisiasa na vitu vingi mno.

Kwahiyo sisi kama jumuiya tukaanza kufikiria hapa hatuitendei nchi yetu haki na kitu cha kwanza tulichokiangalia ni brand ya Tanzania haiku katika level inabidi iwe, ukiangalia binadamu wa kwanza duniani, hicho ni kitu kikubwa, ukiangalia Mlima Kilimanjaro.

Kwa sababu sisi Watanzania kwa sababu ya upole, kuwa wanyenyekevu na kutokaa kuongea hiyo hali ndio imetufikisha hapo na kusema hapana. Kila siku historia yetu sisi Watanzania inazungumzwa na watu wengine. Unakuta Mmarekani amekaa Washington DC anaandika vitu vilivyopo Tanzania, hajawahi kufika Tanzania. Hapo hatuitendei nchi yetu haki.

Kwahiyo tukasema mwaka huu sasa, kuanzia mwaka huu na kuendelea ni kuanza kuiuza nchi yetu ili majirani zetu, watu wanaoishi kwenye miji yetu, kwernye majimbo yetu, kwenye State zetu na kwenye hii nchi kwa ujumla  waweze kujua Watanzania ni nani?

Tunategemea hiyo brand ikianza ikianza kukua watu wataanza kujenga uhusiano, tutaweza kukuza utalii na tutaweza kukuza uchumi. Na kwa kuwatumia hawa wageni waliofika kwenye Tanzania Day, hawa baadaye ndio watakaokuwa wawekezaji tukiweza kuiuza vizuri nchi yetu. Na huo ndio mchango wetu Diaspora.

MTANZANIA: Kwanini Tanzania Day imevumbuliwa na Watanzania wa Dallas Texas pekee na si kwa kuunganisha Watanzania wa miji iliyo karibu na Dallas?

KAZORA : Mawazo yote yalianzia hapa na uongozi wa hapa ndio uliofanya uamuzi. Tukamfuata Meya wa huu mji na kumueleza kuwa sisi tumekuwa na wewe kwa karibu sana kwa muda mrefu na kushirikina nawewe kwa muda mrefu, sasa umefika wakati tuujenge uhusiano wetu na ndio Aprili 29, mwaka jana, akatambua kuwa April 29 kila mwaka itakuwa ni Tanzania Day hapa Dallas. Kwahiyo sio kitu cha sherehe tu ni kitu ambacho kinajulikana maalumu.

MTANZANIA: Huoni kwamba mtakuwa mmewanyima nafasi wale Watanzania walio katika miji mingine?

Kazora: Kwa sababu Dallas wameanzisha kitu haimaanishi ni Dallas peke yao. Watanzania wan chi nzima wamealikwa, waliokuwa Dallas, Texas na nje ya Marekani. Kwahiyo mwaliko ulifika kwa jumuiya zote duniani, Stockholm na hata Dubai, issue sio location cha muhimu ni kuangalia tumekuja kufanya nini.

Mtanzania: Je, mmepata ushirikiano wa kutosha?

Kazora: Changamoto hazikosi na zaidi labda ile concept yenyewe kuielewa na wakati mwingine wewe ukiwaza Tanzania Day mwenzako yeye anawaza ataishi wapi? Atalala wapi? Kwahiyo changamoto ni lazima zitakuwapo na hususani kitu chenyewe kinafanyika kwa mara ya kwanza kinakuwa ni kigumu kwa sababu tunajaribu kubadilisha utamaduni na fikra za watu kwa hiyo ni kitu kigumu.

Kwahiyo watu wengi watajaribu kuona kama itawezekana au ni kitu chenye kuleta tija lakini pole pole mara Gavana katuma barua ya kutambua hii kitu na kushukuru, mara Seneta naye katuma ya kwake, Balozi wa Marekani naye katuma ujumbe wake. Kwahiyo watu wakiona hivi vitu wanawaza hebu nifikirie kwa mara ya pili. Ukitoa hizo changamoto. Kwa sababu hiki kitu ni mara ya kwanza kufanyika basi naweza kusema imefanikiwa.

MTANZANIA: Wewe ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, zipo jitihada zozote unafanya kuwaunganisha viongozi wa miji mingine huko Marekani kuwa na sauti moja ili Tanzania Day iwe na maana halisi kwa kuunganisha Watanzania zaidi?

KAZORA: Kam Mwenyekiti wa Dallas nimebahatika kuwa kwenye kamati kuu ya viongozi wa      Diaspora Duniani. Kati ya watu tisa  kutoka mabara yote mimi ni mmoja wao ninaowakilisha Marekani kwenye hiyo kamati. Lakini pia kwenye maandalizi ya shughuli kama Tanzania Day viongozi wengine wote walishirikishwa kuanzia mwanzo hadi mwisho ndiyo maana shughuli yetu ilikuwa na watu kutoka majimbo 22 ya hapa Marekani peke yake. Kutokana na mtandao tulionao wa Diaspora duniani, shughuli ya Tanzania Day ilikuwa na ushirikianono wa nchi 183.

MTANZANIA: Jumuiya yenu ina miaka mingapi sasa?

KAZORA:  Jumuiya yetu ilianza kutambuliwa na Serikali ya Marekani rasmi kuanzia mwaka 2009.

MTANZANIA: Mmewahi kutoa michango yoyote kusaidia Watanzania wa hapa nyumbani katika majimbo, kata au wilaya?

KAZORA:  Michango yetu imekuwa mingi sana over the years. Kuna kituo cha watoto yatima kilichopo Mkoa wa Kilimanjaro ambacho wanajumuiya wa Dallas wamejitolea kuchangia. Ila pia jumuiya imeanzisha jitihada za kujenga uhusiano wa kudumu kati ya mji wetu na nchi yetu ili kukuza biashara, uwekezaji na utalii. Na zaidi Watanzania waishio Dallas waliitikia wito wa Rais Magufuli wa kutaka Direct flights  kwenda Tanzania kwa kuanzisha maongezi kati ya American Airlines na  chi yetu. Mifano ya jitihada hii ni mingi na inagusa sekta nyingi za nchi yetu.

 MTANZANIA: Watanzania mnaoishi Marekani inaaminika mnatoa mchango mkubwa katika familia kusiaidia ndugu zenu, mewahi kufikiria sasa  kama jumuiya kujitolea kusaidia maendeleo ya nchi kwa jumla?

KAZORA:  Kama wana Dallas tumeishawahi kupeleka wawekezaji nyumbani. Zaidi tunaandaa forums za kuzungumzia fursa za uwekezaji nyumbani. Kikubwa zaidi ni shughuli kama Tanzania Day ambazo zinasaidia mamilioni ya Wamarekani kuanza kujua kuhusu Tanzania na utalii zaidi.

MTANZANIA:  Mliweza kuitangaza Tanzania Day huko katika vyombo vya habari vya Marekani?

KAZORA:  Maandalizi ya Tanzania Day yalihusisha redio na televisheni  za hapa ambazo zinafikiwa na mamilioni ya Wamarekani.

MTANZANIA: Unafikiri Tanzania DAY  peke yake inaweza kuhamasisha Serikali ya Tanzania kuona kuwa wapo Watanzania wanaothamini Utanzania wao?

 KAZORA: Tanzania Day peke yake kweli haitoshi kuonyesha mchango wetu ila ujumla wa jitihada zetu wa mwaka mzima kama kuanzisha discussions za direct flights kutoka hapa hadi nyumbani. Pia tumeunda kamati ya kusaidia kukuza sekta  ya afya na tunaongea na hospitali moja hapa kuona kama wanaweza kufungua kitengo hapo nyumbani. Pia tuko kwenye mazungumzo na chuo kimoja hapa Dallas kusaidia kutoa udhamini wa masomo kwa  Watanzania  hususani  kwenye  eneo la sheria za mafuta na gesi.

MTANZANIA: kuna mtazamo ulio hasi juuya Diaspora kwamba ni watu wanaotumiwa kuharibu siasa za nchi, hili wewe unaweza kulifafanua vipi?

KAZORA:  Mtazamo wa Diaspora kuwa wanaharibu nchi  zaidi ni propaganda kuliko ukweli.  Hapo juu nimetoa mifano kadhaa ya jitihada zetu. Labda cha kuzungumzia zaidi ni kwa nini Serikali ya Tanzania bado haijakumbatia Diaspora wake kama nchi zingine. Diaspora ni development partners wakubwa na ni asset ambayo nchi yetu bado haijaona. Nchi kama Israel na India ni mfano mzuri wa maendeleo kupitia ushirikiano wa Diaspora na nchi yake.

MTANZANIA:  Tanzania Day imefanikiwa? Mmekaa na kufanya tathimini kwamba lengo lenu limefanikiwa?

KAZORA: Tanzania day imefanikiwa sana. Kuona kwamba tumefikia nchi  kwa muda mfupi na bajeti  ndogo ni mafanikio kubwa sana. Naamini matangazo yetu na matumizi ya teknolojia yameonyesha manufaa ya Diaspora na teknolojia kufikisha ujumbe mbali sana kwa gharama nafuu zaidi.

Tanzania Day tulifanikiwa  kwa kuwa tunayo  timu ya uongozi imara sana iliyojaa watu wenye vipaji vingi na uzoefu mkubwa kwenye shughuli kama hizi. Kubwa zaidi ni kwamba tunao wanaharakati wengi ambao wanayo  nia ya kutoa mchango wao kwenye maendeleo ya nchi yetu.

MTANZANIA: Neno lako kwa Diaspora wa mataifa mbalimbali duniani hususani waweze kuona sasa umuhimu wa kusaidia Watanzania wenzao wenye uhitaji hapa nyumbani.

KAZORA:  Neno langu ni kwamba Diaspora ya Marekani na dunia kwa jumla sasa tumeanza kukomaa, tumeelimika na tuna stability ya uchumi. Imefika sasa muda wa kuungana pamoja tuweze kutumia ujuzi na  utaalamu  wetu  kukuza  nchi zetu. Imefika muda pia wa Serikali yetu kuanza kutafakari mbinu kama Diaspora bonds ili kuweza kuondokana na misaada ya wageni na kupata misaada ya Watanzania tulio nje ili kujenga nchi yetu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles