25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

NASH MC AUZA NAKALA ZAIDI YA 100 UJERUMANI

BAYREUTH, UJERUMANI


MSANII wa hip hop anayetamba na wimbo wa ‘Shujaa’, Nash Mc, baada ya onyesho lake katika mji huo ameuza nakala zaidi ya 100 za kazi zake mbalimbali za muziki kwa wadau mbalimbali wa Kiswahili waliohudhuria kwenye Kongamano la 25 la Kiswahili la Chuo Kikuu cha Bayreuth, lililofanyika nchini Ujerumani.

Msanii huyo kutoka Tanzania amekuwa  wa kwanza wa hip hop kutoka Afrika Mashariki kupata nafasi kuhudhuria kongamano hilo na kupata nafasi ya kutumbuiza. 

Nash alisema baada ya kumaliza kutumbuiza alilazimika kuuza nakala zaidi ya 100 za kazi zake mbalimbali za muziki, kutokana na mahitaji ya muziki wake kwa idadi kubwa ya watu waliohudhuria kongamano hilo lililofanyika kwenye jumba la Iwalewa.

“Nafasi iliyopatikana nimeitumikia vizuri, nilifurahi sana baada ya kuona wataalamu wengi wakishuhudia onesho langu na pia kununua zaidi ya nakala 100 baada ya tukio hilo, pia nafurahi kukutana na kubadilishana mawazo na maprofesa wakubwa waliobobea katika fani ya lugha na falsafa kama Prof. Euphrase Kezilahabi, Prof. Odhiambo, Dk. Tom Mboya Lutz Digner na wengine wengi,’’ alisema Nash Mc.

Nash alisema kupitia wataalamu hao kazi yake ya muziki itasambaa kwenye vyuo nikuu wanavyofundisha kwa maana ya kuzitumia nyimbo zake kwenye tafiti zao zitakazohusiana na lugha.

“Pia nawashukuru wataalamu wote kutoka Tanzania tuliokuwa pamoja nao akiwamo Dk. Shani Omari, Hadija Jilala, Sekwiha Idd Mwimbe na wengine wengi kwa ushirikiano wao kwangu,’’ alisema Nash Mc.

Nash MC ni nani?

Ni mfuasi mzuri wa misingi ya hip hop aliyemaliza kidato cha nne mwaka 2003 Shule ya Benjamin William Mkapa, lakini hakuendelea na masomo ya juu.

Baba yake alifariki mwaka 1999, alipokuwa nyumbani bila kazi alikumbuka kipaji chake cha muziki akaamua kujifunza kwanza misingi ya muziki anaoupenda wa hip hop kwa zaidi ya miaka sita, baada ya hapo alianza kuonekana kwenye matamasha mbalimbali ambapo pia alikuwa akitumika kuelezea misingi ya hip hop kwenye vipindi mbalimbali vya redio na Tv.

Mwaka mmoja baadaye, alikutana na waasisi wa muziki wa hip hop nchini, Zavara na Lindu, wakampa miongozo zaidi katika safari yake ya muziki na mwaka 2000 akarekodi wimbo wake wa kwanza wa ‘Nani mkali kwenye game’ chini ya prodyuza Kita wa Rama records.

Nash Mc pia aliwahi kurekodi na kundi la Gorrila Killer ambao kwa sasa wanajiita Pingu na Deso, pia mwaka 2002 alirekodi wimbo mwingine akiwa na Dully Sykes na Dogo Lecha huko FM Records chini ya prodyuza Miika Mwamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles