24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WASHINDI SHINDANO LA FILAMU KUZOA MILIONI 15

Na FESTO POLEA, DAR ES SALAAM



WASHINDI wa Shindano la Filamu kwa vijana (European Youth Film Competition) lililozinduliwa juzi na Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi, Ufaransa, taasisi ya Alliance Francaise pamoja na kituo cha British, watazoa zaidi ya Sh milioni 15.


Shindano hilo litaendeshwa kwa wiki tatu na litahusisha vijana wenye umri kati ya 18 na 35 kutoka Tanzania Bara na Visiwani chini ya kauli mbiu: ‘Ukuaji wa idadi ya watu: Je, hii ni changamoto au fursa? Ambapo mshindi wa kwanza atapata Sh milioni 7 wa pili atapata Sh milioni 5 na mshindi wa tatu atajinyakulia Sh milioni 3.


Kiongozi wa umoja huo nchini Tanzania, Balozi Roeland van de Geer, amesema kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa idadi ya watu, hii inaleta changamoto pamoja na fursa katika shughuli za maendeleo na ni nafasi ya kipekee kwa vijana wa Kitanzania kuonesha ubunifu wao kwenye eneo husika ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania. 


Shindano hili linalotaka filamu fupi kati ya dakika 5 hadi 10, awamu ya kwanza imeanza Mei 29 hadi Juni ikihusisha kupokea ingizo kwenye shindano, fomu za maombi zinapatikana Alliance Francaise, British Council na Bodi ya Filamu Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles