29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MIJI YENYE VYUO BORA 2017

Na FARAJA MASINDE



MAFANIKIO ya kimasomo kwa mwanafunzi yamekuwa yakichangiwa na vitu vingi huku mazingira ikiwa ni kichocheo muhimu.
Tumekuwa tukishuhudia kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakisoma kwenye mataifa ambayo yanakabiliwa na machafuko hata vyuo vyake vimeshindwa kufanya vizuri na hivyo kufanya mji kupoteza hadhi yake kitaaluma.


Pia kumekuwapo mataifa ambayo yamekuwa yakijidhatiti kwa kiwango kikubwa katika kuhakikisha kuwa yanavutia wanafunzi wa kigeni kuja kusoma kwenye vyuo vyao ambapo yamekuwa yakiweka mazingira rafiki kadri inavyowezekana kwa lengo moja tu la kuhakikisha kuwa yanakuwa kivutio.


Hata hivyo, kila mwaka mashirika mbalimbali yanayojihusisha na tafiti za elimu yamekuwa yakitoa ripoti za kila mwaka juu ya ni miji au nchi gani ambazo zina mazingira rafiki kwa mwanafunzi kuweza kusoma vizuri bila ya kuwa na changamoto yoyote kama vita na mambo mengine.


Shirika la Times Higher Education, tayari limeitaja miji ambayo inaongoza kwa kuwa na vyuo bora duniani ambavyo mwanafunzi anaweza kusoma kirahisi kwa mwaka huu wa 2017.


Katika utafiti huo ambao ulifanyika kwenye chuo kilichoko Toronto Canada cha Martin Prosperity Institute na kubainisha  miji ambayo mwanafunzi anaweza kusoma kwa mafanikio makubwa kulingana na ubora wa vyuo na vyenye mazingira rafiki.


Baadhi ya miji hiyo na vyuo vyake ambavyo nafasi zake kwenye 100 bora duniani ziko kwenye mabano nipamoja na hii ifuatayo.
Mji ulioshika namba moja ni Los Angeles ambao umesheheni vyuo vikuu vya California Institute of Technology (2), University of California, Los Angeles (14), University of Southern California (60) na kile cha University of California, Irvine (98).


Mji mwingine ni London Uingereza ambao umetajwa kuwa na vyuo vikuu bora vya Imperial College London (8), University College London (15), London School of Economics and Political Science (25) na King’s College London (36).


Nafasi ya tatu kwenye miji hiyo ni ule wa Hong Kong ambao kuna vyuo bora vya University of Hong Kong (43), Hong Kong University of Science and Technology (49) na Chuo Kikuu cha  Chinese University of Hong Kong (76).


Boston-Cambridge ambao umetajwa kuwa na vyuo vikuu bora vya Massachusetts Institute of Technology (5), Harvard University (6) na kile cha Boston University (64) pia kuna mji mwingine wa Berlin ambao una vyuo vikuu bora vya Humboldt University (57), Free University of Berlin (75), Technical University of Berlin (82).


Mji mwingine uliotajwa ni pamoja na Beijing ambao una vyuo vikuu bora vya Peking University (29) na Tsinghua University (35). Kwenye mji wa New York wenyewe una vyuo bora vya Columbia University (16) na NYU(32).


Pia katika mji wa Chicago, kuna vyuo bora vya University of Chicago (10) na Northwestern University (20).
Miji mingine iliyosalia ambayo imetajwa kwenye orodha hii ya miji yenye vyuo vikuu bora duniani kwa mwaka 2017 ni pamoja na ule wa Singapore, Atlanta, Sydney, Melbourne, Pittsburgh na Stockholm.


Miji mingine ni pamoja na Munich, Liège, The Hague, Durham-Chapel Hill na Utrecht.
Hata hivyo, kwa mujibu wa THE waliohusika na utafiti huo wamebainisha kuwa kwa mwaka huu hakuna tofauti kubwa sana ikilinganishwa na mwaka jana.


Kwani miji hiyo inaelezwa kuwa ndiyo imekuwa ikikimbiliwa na wanafunzi wengi duniani kutokana na kuwa na vyuo bora vinavyofanya vyema katika nyanja mbalimbali za kitaaluma.


Huku miji ya London, Los Angeles, Boston na Berlin ikielezwa kupewa kipaumbele kikubwa zaidi na wanafunzi.
Utafiti huo umevielezea vyuo vikuu vilivyoko kwenye miji mingine ya Atlanta, Pittsburgh, Stockholm na Beijing kuwa ni miongoni mwa vyuo vizuri zaidi duniani.


Miji isiyokuwa na majina makubwa kama Utrecht inatajwa kuipiku miji maarufu ya  Paris na mingine

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles