26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

TEMER ASHINIKIZWA AACHIE MADARAKA

RIO DE JANEIRO, BRAZIL


WANANCHI wa Brazil wamefanya maandamano makubwa ya kumshinikiza Rais Michel Temer ajiuzulu baada ya Mahakama Kuu kutoa amri ya kumchunguza kutokana na kuhusishwa na rushwa.

Madai yanayomkabili Rais Timer yamelitumbukiza taifa hilo kubwa Amerika Kusini katika mzozo kwa mara nyingine tena.

Rais Temer analaumiwa pia kwa visa vinavyohusu rushwa, hali ambayo inazihujumu juhudi za Serikali yake za kujiondoa kwenye hali mbaya ya uchumi katika historia ya Brazil.

Maandamano hayo yalifanyika katika miji tofauti ikiwamo Sao Paulo na Rio de Jenairo, ambako mamia ya waandamanaji walitembea kando mwa fukwe za bahari wakiimba na wengine wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa ‘Temer Nje!’.

Maandamano hayo yamesababisha kushuka kwa sarafu ya nchi hiyo na pia hasara kwenye soko la hisa. 

Mzozo huu mpya sasa umesababisha kuzorota kwa mageuzi kadhaa yaliyowekwa kuisaidia Brazil kutoka kwenye hali mbaya ya uchumi wake ulioporomoka.

Haya yanatokea mwaka mmoja ukiwa haujatimia tangu Rais Temer achukue madaraka baada ya mtangulizi wae Dilma Rousseff, kuvuliwa madaraka kwa kashfa kama hizo.

Mmoja wa waandamanaji, alisema alitegemea hali ingeimarika baada ya Rousseff kuondolewa madarakani, lakini sivyo ilivyokuwa.

Alisema Wabrazil lazima wafikirie upya wakati wa kupiga kura kwenye uchaguzi ujao ili kuweza kuwachagua viongozi wazuri katika siku za usoni.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles