HII ni aina ya ngiri ambayo inatokea tu bila kuhusisha kasoro za kuzaliwa nazo. Mara nyingi hutokea kama matokeo ya mgandamizo wa hewa au nguvu ndani ya tumbo.
Sababu kuu ya ugonjwa huu ni pamoja na unene kupita kiasi, kunyanyua vitu vizito mara kwa mara, kikohozi kisichoisha, pia ujauzito wa mapacha kwa mwanamke au kupata ujauzito kila mara kunaweza kusababisha mtu kupata aina hii ya ngiri.
Hii ni aina ya ngiri ambayo huwapata zaidi watoto wadogo mpaka miaka mitano ingawa watu wazima pia wanaweza kupatwa na ngiri ya aina hii. Kwa kawaida kitovu hujitokeza nje. Hii hutokana na misuli ya tumbo kuachana kidogo.
Dawa ya asili ya ngiri ya kitovu
Kitovu ambacho hujitokeza nje (ngiri kitovu) husababishwa na misuli ya tumbo kuachana kidogo. Kwa watoto wadogo aina hii ya ngiri huwa haihitaji dawa na hutoweka yenyewe na endapo inaendelea hata baada ya miaka mitano basi matibabu yanaweza kuhitajika ikiwamo upasuaji.
Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi
Nyuzinyuzi hupatikana katika karoti, matunda aina zote hasa parachichi, kabeji, mboga za majani, jamii ya kunde, mbegu za maboga, mahindi mabichi, ugali wa dona, viazi n.k.
Asilimia 80 ya chakula chako kwa siku itokane na vyakula katika makundi haya. Mtindo huu wa chakula utumike kwa kipindi kirefu mpaka mgonjwa amepona na unaweza kuendelea kuishi hivi kwa afya bora ya mwili wako kwa miaka mingi ijayo.
Aloe vera (mshubiri)
Aloe vera au mshubiri ni moja ya dawa nzuri zaidi za asili kwa matatizo mbalimbali ya tumbo yanayosababishwa na ngiri. Huzisafisha kuta za ndani ya tumbo na kuziwekea ulinzi huku ukiondoa maumivu yoyote ya tumbo. Pia hudhibti kiungulia kirahisi zaidi.
Kunywa ¼ kikombe ya juisi ya aloe vera dakika 20 kabla ya kula chakula cha mchana na cha jioni, unaweza kuchanganya na juisi ya embe au parachichi kufanya kikombe kizima kupunguza ukali wa dawa wakati unakunywa. Usitumie zaidi ya vijiko vikubwa viwili vya jeli (maji maji) ya aloe vera unapoandaa hii juisi yako la sivyo unaweza kupatwa na ugonjwa wa kuharisha.
Unapaswa kuepuka vilevi vyote, vyakula vyenye mafuta mengi na ujishughulishe na mazoezi ya viungo kila siku.
Mwandishi wa makala hii ni Fadhili Paulo ambaye pia ni tabibu wa dawa asili. Anapatikana kwa WhatsApp kupitia namba +255769142586.