26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

JAY Z AGUSWA NA SHOO YA ALI KIBA

NEW YORK, MAREKANI 

SHOO ya OneAfrika aliyoifanya mkali wa muziki nchini Tanzania, Ali Kiba, nchini Uingereza mwishoni mwa wiki alipotumia bendi, imemvutia rapa Jay Z kiasi cha mtandao wa rapa huyo, Tidal unaoshugulikia masuala ya muziki kuposti video ya Ali Kiba akiwa jukwaani akipiga shoo hiyo.

Mtandao huo uliandika: “Asiyezuilika, Official Alikiba moja kwa moja anafanya shoo kwa sasa mjini London.”

Ali Kiba alikuwa miongoni mwa wasanii wa Afrika waliopiga shoo hiyo na kuwapagawisha mashabiki waliojitokeza kwenye uwanja wa Wembley na wale waliokuwa wanafuatilia kupitia mitandao ya kijamii.

Hiyo ni hatua kubwa kwa Ali kiba kupostiwa video yake kwenye mitandao mikubwa ya muziki duniani. 

Baadhi ya wasanii wengine ambao walikuwa kwenye shoo hiyo lakini hawakupostiwa kwenye mtandao huo ni pamoja na P-Square, Davido, Wizkid, Tiwa Savage na wengine wengi.
 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles