Watafiti nchini Uingereza wanasema dawa za kupunguza makali ya virusi katika Ulaya na Amerika ya Kaskazini zimeboreshwa kiasi kwamba watu mwenye Virusi vya UKIMWI wanaweza kuishi kwa karibia sawa tu na watu wengine wasio na virusi.
Wanasayansi kutoka Chuo kikuu cha Bristol, waliwachunguza watu wenye virusi vinavyosababisha UKIMWI wapatao elfu tisini. Makadirio yao yanaonesha kuwa mtu mwenye umri wa miaka 21 aliyeanza matibabu mwaka 2008 au baadaye anaweza kuishi mpaka kufikia umri wake wa miaka 70.
Zaidi ya watu milioni mbili wanaishi na Virusi vya UKIMWI katika Ulaya na Amerika Kaskazini.
Kwa upande wa Takwimu za ulimwengu, watu walioathirika na virusi hivyo ni milioni 36 wengi wao wakiwa barani Afrika.