27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAAGIZA SUKARI NJE YA NCHI

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa

 

 

Na MAREGESI PAUL-DODOMA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewatoa hofu Watanzania kwamba sukari itaendelea kupatikana kwa wingi wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan unaotarajia kuanza baadaye mwezi huu.

Amesema kwamba, bidhaa hiyo lazima iwepo wakati huo kwa kuwa ni muhimu na inahitajika zaidi wakati wa mfungo huo.

Waziri Mkuu Majaliwa, alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Jaku Hashim Ayoub  (CCM), aliloliuliza wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.

“Mheshimiwa Jaku umezungumza mambo mengi kwenye swali lako, lakini la msingi zaidi ni kuhusu sukari.

“Kwa kifupi ni kwamba, mahitaji ya sukari katika nchi yetu katika msimu wa kilimo ni tani 420, lakini uzalishaji ni tani 320.

“Kutokana na hali hiyo, tumekuwa tukiagiza sukari kutoka nje na ushahidi wa hilo ni kwamba tumeagiza tani 80 kutoka nje na hadi sasa tani 35 zimeshawasili bandarini.

“Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, sukari itakuwepo ya kutosha wakati wote na hakuna haja kwa wananchi kuwa na hofu kwa sababu Serikali ina mipango ya kuongeza uzalishaji kupitia viwanda vyetu vya Mtibwa, Kilombero, TPC, Kagera Sugar na vingine vinavyoanzishwa.

“Lakini, nawaomba wanaopandisha bei ya sukari bila sababu waache tabia hiyo kwa sababu hakuna sababu ya kufanya hivyo,” aliagiza Waziri Mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles