25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

VIJANA NIGERIA WAONGOZA KUSAKA ELIMU NG’AMBO

Wanafunzi wa Kinegeria wanaosoma ng’ambo

 

NA JOSEPH LINO,

VIJANA kutoka Afrika wamekuwa na hamasa kubwa kwenda kusoma taaluma mbalimbali hasa Bara la Ulaya na Marekani.

Kuongezeka kwa wanafunzi wa ngazi ya elimu ya juu, baadhi ya nchi za Afrika wamekuwa na shauku kubwa ya kuwa na idadi kubwa wanafunzi wa kimataifa.

Ripoti ya UNESCO Institute for Statistics (UIS) inaonesha kuwa nchi za Afrika zinaongoza kuwa na wanafunzi wengi wa kimataifa katika mabara mengine duniani.

Wanafunzi kutoka mataifa ya Afrika 54 kwa ujumla, hadi kufikia mwaka 2013,  asilimia 10 ni Waafrika.

Kuanzia mwaka 2006 hadi 2014, idadi ya wanafunzi kutoka Afrika ambao wanasoma Shahada ya kwanza katika mabara mengine imeongezeka kwa asilimia 24 kutoka  343,370 hadi 427,311.

Kwa mujibu wa ripoti ya UIS nchi ya Nigeria inaongozwa kuwa na wanafunzi wengi ambao wanasoma vyuo vikuu nje ya Afrika.

Nigeria ina wanafunzi wa elimu ya juu takribani milioni 1.4 nchini humo, lakini wanafunzi wa kimataifa wanafikia 71,351 ambao wanasoma Shahada ya kwanza nje.

Idadi ya wanafunzi kutoka Nigeria imekuwa ikiongezeka kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 ambapo waliongezeka kwa asilimia 45.

Nchi nyingi ambazo wanafunzi wa Nigeria hupendelea kwenda kusoma ni pamoja Uingereza, Ghana na Marekani.

Hata hivyo, robo ya wanafunzi wote wa kimataifa wanaosoma nchini Marekani wanatoka Nigeria.

Nayo Morocco ilikuwa miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zina idadi kubwa ya wanafunzi wa Kimataifa. Ripoti ya UIS inaonyesha kuwa wanafunzi kutoka Morocco ni 43,148 ambao walikuwa wamesajiliwa katika vyuo vikuu mbalimbali ambapo wanafunzi 25,000 walikwenda kusoma Ufaransa na 5,700 walikwenda kusoma Hispania na Ujerumani.

Kwa upande wa Cameroon wanafunzi 23,131 walienda kusoma ng’ambo wakichukua Shahada kati ya wanafunzi 245,000 wa elimu ya juu nchini humo.

Asilimia 69 ya wanafunzi hao 15,474 wanasoma vyuo vikuu vya Ulaya kama Ujerumani, Ufaransa  na Ubelgiji na asilimia 5.5 ambayo ni wanafunzi 1,268 ambao walienda kusoma Marekani. Algeria wanafunzi 20,493  walienda kusoma nje ambapo asilimia 81 ya wanafunzi hao ambayo ni 16,558 wanasoma shahada ya kwanza katika vyuo vya Ufaransa.

Aidha, Zimbabwe ni wanafunzi 16,563 ambao walienda kusoma shahada nje ya nchi hiyo, ambapo wanafunzi 10,000 wanasoma Afrika Kusini na wanafunzi 1,268 wanasoma vyuo vikuu vya Marekani.

Kenya, wanafunzi 13,024 wa Shahada ya kwanza walienda kusoma vyuo vya nje ikiwa Marekani peke yake wanafunzi 3,177 walijisajili katika vyuo hivyo, hii inamaanisha kwamba wanafunzi wa kimataifa wanapendelea kusoma elimu ya juu nchini Marekani.

Wanafunzi wengine walienda kusoma Uingereza, Australia na Afrika Kusini.

Senegal ilipeleka wanafunzi  11,410 kusoma nje ambapo 7,439 walienda kusoma Ufaransa na wengine 700 walienda nchini Marekani.

Angola ilikuwa na wanafunzi 11,121 walienda kusoma nje hasa katika nchi za Brazil, Ureno, Marekani na baadhi ya nchi za Afrika zikiwamo Gambia na Afrika Kusini, ambapo Ghana ilikuwa na wanafunzi wa kimataifa 11,116 wengi wao walikwenda Marekani kama wanafunzi 3,142. Pia Sudan ilikuwa wanafunzi wa kimataifa 10,058 ambao walienda kusoma Shahada ya kwanza nje.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles