30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

BAYERN MUNICH WATANGAZA UBINGWA UJERUMANI

MUNICH, UJERUMANI


KLABU ya Bayern Munich imefanikiwa kutangazwa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Ujerumani kwa mara ya tano mfululizo, baada ya juzi kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya wapinzani wao, Wolfsburg.

Mabingwa hao wapya wameweza kutangaza ubingwa ikiwa ni saa chache baada ya wapinzani wao kwenye msimamo wa Ligi, Leipzig, kutoka suluhu dhidi ya Ingolstadt na kuwafanya Bayern Munich watangaze ubingwa kwa tofauti ya pointi 10, huku ikiwa imebaki michezo mitatu kumalizika kwa Ligi.

Katika mchezo huo, dakika 45 za kipindi cha kwanza Bayern Munich walikuwa mbele kwa mabao 3-0, yaliyowekwa wavuni na David Alaba, Robert Lewandowski akifunga mawili kabla ya Arjen Robben, Thomas Muller na Joshua Kimmich kuongeza mabao matatu kipindi cha pili.

Kiungo wa zamani wa Bayern Munich, Luis Gustavo, raia wa nchini Brazil ambaye kwa sasa anakipiga katika kikosi cha Wolfsburg, alioneshwa kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu na baadaye kutaka kumshambulia mwamuzi.

Kocha wa klabu ya Bayern Munich, Carlo Ancelotti, amejiwekea historia katika klabu kubwa barani Ulaya kutwaa mataji ya Ligi, ikiwa pamoja na nchini Italia, England na Ufaransa.

Ancelotti, ambaye alifukuzwa na klabu ya Real Madrid, Mei 25, 2015, amewashukuru mashabiki wa Bayern Munich kwa ushirikiano waliouonesha tangu kujiunga kwake ndani ya kikosi hicho Julai 2016.

“Ni muda wa kufurahia ubingwa, ni kazi ambayo imefanywa na wote, ikiwa pamoja na mashabiki, wachezaji, viongozi pamoja na wadau mbalimbali wa soka ndani ya klabu hii, tunayo furaha kubwa msimu huu kwa hapa tulipofikia.

“Nawashukuru mashabiki kwa sapoti yao kwa kipindi chote hadi kufikia hapo, umoja wao umewafanya wachezaji kujisikia kuwa na furaha mara kwa mara katika michezo yao kutokana na sapoti waliyopata,” alisema Ancelotti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles