32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI KUIBANA KOREA KASKAZINI IREJEE MEZA YA MAZUNGUMZO

WASHINGTON, MAREKANI


SERIKALI ya Marekani imeahidi kuibana zaidi Korea Kaskazini, kuilazimisha kurejea kwenye meza ya mazunguzo kuhusu programu yake ya nyuklia na imesema hailengi kuuangusha utawala wa Kim Jong-Un.

Msimamo huo wa Marekani, ambao ulionekana kuashiria utayari wa kumaliza njia zote zisizo za kijeshi licha ya onyo za mara kwa mara, kwamba njia zote zinazingatiwa, umekuja kufuatia mkutano usio wa kawaida katika Ikulu ya Marekani, ukihusisha wajumbe wote wa Baraza la Seneti.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje, Rex Tillerson, Waziri wa Ulinzi, Jim Mattis na Mkurugenzi wa Idara ya Intelijensia, Dan Coats, iliielezea Korea Kaskazini kama kitisho kikubwa cha usalama wa taifa na kipaumbele cha sera ya kigeni.

Mmoja wa maseneta waliohudhuria mkutano huo, Chris Coons kutoka chama cha Democrat, alisema wabunge hawakupewa maelezo kuhusu njia mahususi za kijeshi au kuombwa kuidhinisha shambulio, bali maelezo ya busara juu ya namna ya kushughulika na Korea Kaskazini.

“Nimetiwa moyo kwamba waliamua kulitolea maelezo baraza zima la Seneti. Yalikuwa maelezo yenye busara na ilibainishwa wazi si rahisi kuingia mkenge wa shambulio la kijeshi bali mkakati wa kipaumbele ni wa diplomasia," alisema Seneta huyo wa Delaware.

Kitisho cha nyuklia na makombora kutoka Korea Kaskazini, kinaelezwa kuwa changamoto nzito zaidi ya kiusalama inayoukabili utawala wa Rais Donald Trump kwa wakati huu.

Trump ameahidi kuizuia Korea Kaskazini kuwa na uwezo wa kuishambulia Marekani kwa kutumia kombora la nyuklia, uwezo ambao wataalamu wanasema inaweza kuupata baada ya mwaka 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles