28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

MERKEL: NI NDOTO ZA MCHANA UINGEREZA KUPATA UPENDELEO EU

BERLIN, UJERUMANI


KANSELA wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema Uingereza isiishi katika mawazo ya kufikirika, kwamba itakuwa na haki zilezile kama wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) baada ya kujitoa kutoka chombo hicho.

Merkel ameyasema hayo bungeni hapa jana na kuongeza kuwa Uingereza itakuwa kama mshirika tu, na haitapata haki kama taifa mwanachama.

Taarifa hiyo ya Merkel imekuja kabla ya mkutano utakaofanyika kesho kuhusu kujitoa kwa Uingereza (Brexit) mjini Brussels, Ubelgiji.

“Hii inawezekana kuonekana kama  kujipendelea, lakini ni lazima niseme wazi kwa sababu baadhi ya watu nchini  Uingereza wanaonekana kuwa na ndoto za  mchana kuhusu suala hili.

“Wapenzi ndugu zangu, huenda mnaweza kufikiria kwamba hili ni jambo la kawaida tu. Lakini kwa bahati mbaya naweza kusema wazi, napata hisia baadhi ya watu nchini Uingereza wana mawazo ya  kufikirika. Hii ni kupoteza muda,” alisema Merkel.

Alisema mazungumzo ya mwanzo kuhusu Brexit ni lazima yajumuishe majukumu ya kifedha ya Uingereza, ikiwa ni pamoja na baada ya kujitoa kutoka umoja huo.

Pia alisema masharti ya kujitoa kwa  Uingereza ni lazima yafikiwe katika njia  inayoridhisha, kabla ya majadiliano kuingia katika uhusiano mpya na umoja huo, mtiririko ambao Merkel ameuita kuwa, usioweza kubadilishwa tena.

Viongozi wa mataifa 27 wanachama wa EU watakutana kesho kuweka misingi ya  umoja huo, licha ya kwamba mazungumzo  hayo yataanza rasmi Juni mwaka huu. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,085FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles