Na FERDNANDA MBAMILA,
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Wakala wa Majengo nchini (TBA), inaendelea na ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa umma katika eneo la Bunju Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam.
TBA ni wakala wa majengo ambao hadi sasa wapo nchi nzima katika zaidi ya mikoa 26 ambapo katika kila Mkoa wapo katika shughuli utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa Umma.
Mradi huu ni sehemu ya mradi maalum wa ujenzi wa nyumba 10,000 za makazi ya watumishi wa Umma zinazo tarajiwa kuwa na nyumba 851 za aina mbalimbali kukidhi mahitaji halisi ya Mtanzania.
Mradi umetekelezwa katika awamu ya mbalimbali kwa kila awamu ikiwa na idadi tofauti ya nyumba kulingana na upatikanan ji wa fedha, wawamu hizi ni kama ifuatavyo.
Katika awamu ya kwanza kuna jumla ya nyumba 155 zilizojengwa na kati ya nyumba 25 zilijengwa, wakandarasi binafsi na nyumba 130 zilijengwa na wakala wa majengo kupitia kikosi cha ujenzi (TBA Brigade).
Pia katika awamu hii ya ujenzi wa jumla ya nyumba 160 ulianza ukitekelezwa na kikosi cha ujenzi cha Wakala wa Majengo nchini, TBA.
Hata hivyo, kati ya nyumba 96 zilitarajiwa kujengwa kwa teknolojia ya kisasa yenye kutumia muda mfupi na gharama ndogo zadi iitwayo “TUNNEL FORM”.
Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga, anasema kazi ya uwekaji msingi wa nyumba hizo ikifuatiwa na ufungaji wa mtambo wa kuhamishia na kunyanyulia mzigo inasubiriwa ili iweze kukamilika.
Zaidi ya nyumba 64 zilijengwa kwa utaalamu wa kawaida, ukizingatia ubunifu, muda na gharama ili kuhakikisha kwamba watumishi wa umma wanapata makazi bora kwa gharama nafuu zaidi, nyumba hizo zipo katika hatua za mwisho tayari kwa kuuzwa.
Mwakalinga anasema, katika awamu ya tatu ya ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa umma jumla ya nyumba 300 zinatarajiwa kujengwa katika utekelezaji huo. Anasema, wakala umetoa kipaumbele kwa nyumba 64 za aina tofauti tofauti, ikiwamo nyumba za ghorofa, bungalo pamoja na nyumba za kujitegemea za familia moja (detached medium house) kufuatia uhitaji mkubwa wa nyumba za aina hiyo.
Idadi ya nyumba zilizokwisha anza kujengwa katika mradi wa nyumba za wananchi za Bunju ni 58. Hii ni idadi pungufu kulingana na ilivyokusudiwa kwasababu wakati wa kuanza ujenzi imeonekana kuwa baadhi ya viwanja vilikuwa vimekwisha endelezwa na watu wengine.
Mwakalinga anabainisha kuwa, maendeleo ya ujenzi yapo katika hatua mbalimbali, ambapo yapo katika hatua ya kitalu kimoja na baada ya kingine kulingana na eneo husika.
Katika awamu ya tatu anasema, kuna vipengele ambavyo kama mkandarasi na msimamizi wa majengo ni lazima azingatie, kama vile ujenzi wa kuta za msingi wa nyumba (foundation wall), urudishaji wa udongo katika mashimo ya msingi (backfilling), ufungaji wa chuma za mkanda wa msingi (plinth beam), ujenzi wa msingi wa kreni ya kunyanyua mzigo au vifaa wakati wa ujenzi wa ghorofa ambao hutumia teknolojia ya ‘tunnel form’ na ujenzi wa mifumo ya majitaka (sewer network and treatment plants).
“Pamoja na hayo, katika awamu ya tatu imejielekeza kujenga na kukamilisha mifumo miwili ya usafirishaji maji taka kwa kutumia teknolojia mpya yenye manufaa makubwa ya ‘DEWATS’,” anasema Mwakalinga.
Anasema kupitia mifumo hiyo yenye kutumia eneo dogo na gharama ndogo, itawanufaisha kwa kiasi kikubwa wakazi wa eneo kwa namna nyingi, ikiwamo utengenezaji wa gesi asilia itakayosaidia katika shughuli mbalimbali.
Pamoja na hayo, kwa yale mabaki yatokanayo na mifumo hiyo, yanaweza kutumika kwa ajili ya mbolea isiyo na madhara na maji kutumika katika shughuli nyingine za uchumi, kama vile umwagiliaji.
Mwakalina anasema, kila kitu kina changamoto zake, hivyo hata katika mradi wa nyumba hizo kuna changamoto mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine hutokea katika maeneo mbalimbali, hasa ya viwanja.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni kama vile watu kujenga nyumba katika baadhi ya viwanja vya eneo la mradi, hali hiyo imechangia uwepo wa upungufu wa idadi ya nyumba zilizokusudiwa, kuchelewa kwa upatikanaji wa malighafi mbalimbali za ujenzi, hasa mawe, hiyo imerudisha nyuma kasi ya ujenzi wa nyumba kuwa endelevu.
Anasema kutokana na watu kujenga nyumba katika baadhi ya viwanja vya eneo la mradi, uongozi katika timu ya mradi umetoa taarifa katika ngazi ya utawala wa juu kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
Vilevile kutokana na kuchelewa kwa upatikanaji wa malighafi mbalimbali za ujenzi, hasa mawe, uongozi wa timu ya mradi TBA umetoa taarifa katika ngazi ya utawala wa juu, hususan idara ya manunuzi kwa ajili ya kuchukua hatua za haraka.
“Wakala wa Majengo unafanya kila aina ya jitihada ili kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapatiwa makazi bora kwa gharama ndogo zitakazowawezesha kumudu kununua nyumba hizo.