27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

VIJANA WATAKIWA KUJITAFUTIA FURSA

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Athony Mavunde
Na HARRIETH MANDARI,

VIJANA nchini wametakiwa kubadili mtazamo wa kuwa ajira ndiyo njia pekee ya kuwainua kiuchumi na badala yake wajikite kwenye sekta isiyo rasmi kwa kuanzisha biashara mbalimbali.

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Athony Mavunde, ameyasema hayo hivi karibuni, wakati akifungua mafunzo ya uhamasishaji wa ujasiriamali kwa vijana wa jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri huyo alisema, bado vijana wengi wana mtazamo kuwa ajira ndiyo njia pekee ya kuwa na maisha bora na ya uhakika.

Alisema takwimu za vijana walio kwenye sekta iliyo rasmi na isiyo rasmi nchini ya mwaka 2014, zinaonyesha vijana walio kwenye sekta rasmi ni kati ya 850,000 -1,000,000,000 na walio bado  kwenye  soko la ajira  ni 150,000-200,000 na hivyo kuweka pengo la vijana zaidi ya 600,000 ambao hawana cha kufanya.

“Kama Serikali, tumekuwa tunachukua hatua kuondokana na changamoto hiyo ambapo imeanza kuwawezesha vijana mmoja mmoja na vikundi,” alisema Mavunde.

Alisema kuwa, tatizo linalokwamisha kundi hilo ni kukosa vigezo vya kukopesheka kwenye mabenki, hivyo kuwalazimu kukaa vijiweni bila kazi, japokuwa wengine tayari wana mawazo na mipango mizuri ya biashara.

“Lipo kundi la vijana ambao pamoja na kuwa hawakufanikiwa kusoma hadi ngazi za elimu ya juu, lakini wana vipaji vya ufundi, kilimo na vingine vingi, ambao pia serikali imeandaa mkakati wa kuwakwamua kiuchumi kupitia vipaji  vyao,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles