33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MRADIWA TBA WAOKOAWATUMISHIWAUMMA

Na FERDNANDA MBAMILA,

SERIKALI  ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Wakala wa Majengo nchini  (TBA), inaendelea na  ujenzi wa  nyumba za makazi ya watumishi wa umma katika eneo la Bunju  Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam.

TBA ni wakala wa majengo ambao hadi sasa wapo nchi nzima  katika zaidi ya mikoa 26 ambapo  katika kila Mkoa wapo katika shughuli utekelezaji wa ujenzi wa  nyumba za watumishi wa Umma.

Mradi huu ni sehemu ya  mradi  maalum wa ujenzi wa nyumba  10,000 za makazi ya  watumishi wa  Umma  zinazo tarajiwa  kuwa na nyumba  851 za aina mbalimbali kukidhi mahitaji halisi ya Mtanzania.

Mradi umetekelezwa  katika  awamu ya  mbalimbali kwa kila awamu  ikiwa na idadi  tofauti ya nyumba kulingana na upatikanan ji wa fedha, wawamu hizi ni kama ifuatavyo.

Katika awamu ya  kwanza  kuna jumla ya nyumba 155 zilizojengwa  na kati ya nyumba 25 zilijengwa, wakandarasi  binafsi  na nyumba 130 zilijengwa na  wakala wa majengo  kupitia  kikosi cha ujenzi (TBA Brigade).

Pia katika  awamu  hii ya ujenzi wa jumla  ya nyumba 160 ulianza  ukitekelezwa na kikosi cha ujenzi cha Wakala wa  Majengo nchini, TBA.

Hata hivyo, kati ya nyumba  96 zilitarajiwa kujengwa kwa teknolojia  ya kisasa yenye kutumia muda mfupi  na gharama  ndogo  zadi iitwayo “TUNNEL FORM”.

 

Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga, anasema kazi ya uwekaji  msingi wa  nyumba hizo ikifuatiwa na ufungaji wa  mtambo wa kuhamishia na kunyanyulia mzigo inasubiriwa ili iweze kukamilika.

 Zaidi ya nyumba  64 zilijengwa kwa utaalamu wa kawaida, ukizingatia ubunifu, muda na  gharama ili kuhakikisha kwamba watumishi wa umma  wanapata makazi bora kwa gharama nafuu zaidi, nyumba hizo zipo katika hatua za mwisho tayari kwa kuuzwa.

Mwakalinga anasema, katika awamu ya  tatu ya ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa umma  jumla ya nyumba 300 zinatarajiwa  kujengwa  katika utekelezaji huo. Anasema, wakala umetoa kipaumbele kwa nyumba 64 za aina tofauti tofauti, ikiwamo nyumba za  ghorofa, bungalo pamoja na nyumba za kujitegemea za familia moja (detached medium house) kufuatia uhitaji mkubwa wa  nyumba za aina hiyo.

Idadi ya nyumba zilizokwisha anza kujengwa katika mradi wa  nyumba za wananchi za Bunju  ni 58. Hii ni  idadi pungufu kulingana na ilivyokusudiwa  kwasababu  wakati wa kuanza ujenzi imeonekana kuwa baadhi ya  viwanja  vilikuwa vimekwisha  endelezwa na watu wengine.

Mwakalinga anabainisha kuwa, maendeleo ya  ujenzi yapo katika hatua mbalimbali, ambapo yapo katika hatua ya kitalu kimoja  na baada ya kingine kulingana na eneo husika.

Katika awamu ya tatu anasema, kuna vipengele ambavyo kama mkandarasi na msimamizi wa majengo ni lazima azingatie, kama vile ujenzi wa kuta za msingi wa nyumba (foundation wall), urudishaji wa udongo katika mashimo ya msingi (backfilling), ufungaji wa chuma  za mkanda wa msingi (plinth beam), ujenzi wa msingi wa kreni ya kunyanyua mzigo au vifaa wakati wa  ujenzi wa ghorofa  ambao hutumia teknolojia ya ‘tunnel form’ na ujenzi wa mifumo ya majitaka (sewer network and treatment plants).

“Pamoja na hayo, katika awamu ya tatu imejielekeza  kujenga na kukamilisha mifumo miwili ya usafirishaji maji taka kwa kutumia teknolojia mpya yenye manufaa makubwa ya ‘DEWATS’,” anasema Mwakalinga.

Anasema kupitia mifumo hiyo  yenye  kutumia eneo dogo na gharama ndogo, itawanufaisha kwa kiasi kikubwa wakazi wa eneo kwa namna nyingi, ikiwamo utengenezaji wa gesi asilia itakayosaidia katika shughuli mbalimbali.

Pamoja na hayo, kwa yale mabaki yatokanayo na  mifumo hiyo, yanaweza kutumika kwa ajili ya mbolea isiyo na madhara na maji kutumika katika shughuli nyingine za uchumi, kama vile umwagiliaji.

Mwakalina anasema, kila kitu kina changamoto zake, hivyo hata katika mradi wa nyumba hizo kuna changamoto mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine hutokea katika maeneo mbalimbali, hasa ya viwanja.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni kama vile  watu kujenga nyumba katika baadhi ya viwanja vya eneo la mradi, hali hiyo imechangia uwepo wa upungufu wa  idadi ya nyumba zilizokusudiwa, kuchelewa kwa upatikanaji wa malighafi mbalimbali za ujenzi, hasa  mawe, hiyo imerudisha nyuma kasi ya ujenzi wa nyumba kuwa endelevu.

Anasema kutokana na watu kujenga nyumba katika baadhi ya viwanja vya eneo la mradi, uongozi katika timu ya mradi umetoa taarifa katika ngazi ya utawala wa juu kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.

Vilevile kutokana na kuchelewa kwa upatikanaji wa malighafi mbalimbali za ujenzi, hasa mawe, uongozi wa timu ya mradi TBA umetoa  taarifa  katika ngazi ya utawala wa juu, hususan idara ya manunuzi kwa ajili ya kuchukua hatua za haraka.

“Wakala wa Majengo unafanya kila aina ya jitihada ili kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapatiwa  makazi bora kwa gharama ndogo zitakazowawezesha kumudu kununua nyumba hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles