NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM
ameandaa programu ya timu yake, huku akisisitiza kuwa anataka mazoezi makali ya wiki sita kabla ya kuanza Ligi ya Tanzania Bara, ili kuwaweka sawa wachezaji wake.
Ligi ya Tanzania Bara imepangwa kuanza Agosti, huku ikitarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake, ambapo bingwa mtetezi akiwa ni Azam FC iliyofanikiwa kulitwaa msimu uliopita.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema Logarusic alipendekeza mazoezi yake yawe ya wiki sita kabla ya kuanza ligi, hivyo Kamati ya Utendaji ilitarajiwa kukutana jana jioni kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kuisuka timu yao.
Alisema wanaamini program za kocha wao zitakwenda kama alivyotarajia, kwa ajili ya kuwa na timu imara yenye nguvu itakayoonyesha maajabu katika Ligi.
“Tumewasiliana na Loga na kuafikiana kuwa mazoezi ya timu yetu yatafanyika ndani ya wiki sita, akiamini kuwa yatatosha kabisa kuandaa vijana wake katika patashika ya Ligi Kuu.
“Uongozi umekubaliana na wazo hilo, hivyo tunaamini kuwa Kamati ya Utendaji mpya itajaribu kuangalia mambo mengine ya maana, ili kuiweka Simba katika nafasi nzuri msimu ujao,” alisema.
Loga ataendelea kuwa kocha wa Simba, baada ya Rais wao Evans Aveva kutangaza kuwa hataweza kusitisha kibarua cha kocha huyo, kwa madai kuwa bado ana ari ya kuwanoa vijana wao hao.