24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Okwi asajiliwa KF Tirana Albania

Na Mwandishi Wetu

MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Yanga,

Emmanuel Okwi
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Emmanuel Okwi

ameitosa klabu hiyo na kusajiliwa na klabu ya KF Tirana ya Albania inayocheza ligi Kuu nchini humo, baada ya kushindwa kurudi katika klabu yake kutokana na migogoro iliyojitokeza.

Okwi alikimbia klabu hiyo na kugoma kurudi, akidai kutomaliziwa fedha zake za usajili Sh milioni 60, baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la Sh milioni 160.

Kwa mujibu wa mtandao wa timu hiyo, imeoroshesha jina la Okwi katika orodha ya wachezaji wapya, lakini haikuweka wazi amesaini mkataba wa miaka mingapi kuchezea klabu hiyo inayonolewa na Kocha Gugash Magani.

Mbali na Okwi, wachezaji wengine wa Afrika Mashariki waliopo katika timu hiyo ni Mkenya Francis Kahata, Mnyarwanda Meddie Kagere na Mrundi Seleman Ndikumana.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuleta upinzani kwenye ligi nchini Albania, kutokana na ubora wa wachezaji hao kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kuwa na viwango vizuri.

Okwi amekuwa akitafsiriwa kama mchezaji msumbufu, kutokana na kushindwa kukaa kwa muda mrefu katika klabu anazochezea.

Kabla ya kujiunga na Yanga, Okwi alishindwa kukaa katika klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia alipouzwa na Simba, klabu aliyoichezea kwa miaka miwili kwa Shilingi milioni 480, akidai hawakumpa fedha walizomuahidi kesi ambayo ilifika hadi Shirikisho la soka Duniani FIFA.

Baada ya kutua Yanga Desemba mwaka jana na kucheza kwa nusu msimu, Okwi alitimka tena hivyo klabu pekee ambayo amedumu ni Simba ambayo alijiunga nayo mwaka 2010 hadi 2012 alipouzwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles