26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Luis Suarez akaribia Barcelona

Nyota wa Liverpool, Luis Suarez
Nyota wa Liverpool, Luis Suarez

LONDON, England

MIAMBA ya soka nchini Hispania, klabu ya Barcelona imesema kuwa majadiliano ya usajili wa nyota wa Liverpool, Luis Suarez yanatarajiwa kukamilika baada ya kuandaa kitita cha pauni milioni 80.

Klabu hizo zipo kwenye mazungumzo mazito juu ya Lusi Suarez, ambapo mkurugenzi mtendaji wa Liverpool, Ian Ayre amedaiwa kukubali kukutana na mkurugenzi wa Barcelona, Raul Sanllehi, ambaye ameweka wazi dhamira yao ya kutoa pauni milioni 80.

Hata hivyo, Liverpool imesisitiza kumtaka mshambuliaji wa Barcelona, Alexis Sanchez mwenye thamani ya pauni milioni 20, ambapo Barca itatoa pauni milioni 60 pamoja na nyota wake huyo.

Kwa upande wake Barcelona imesema nyota wake Alexis Sanchez ana thamani ya pauni milioni 35 tofauti na thamani inayotajwa na Liverpool milioni 20.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles